• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Serikali yaahidi kuikarabati Sekondari ya Wasichana Iringa

Imewekwa tar.: May 3rd, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ameahidi kuwa shule ya sekondari ya Wasichana Iringa iliyopo mkoani Iringa itafanyiwa ukarabati ikiwa ni muendelezo wa serikali katika kuzikarabati shule zake kongwe hapa nchini.
Waziri Jafo alitoa kauli hiyo jana wakati akiwa njiani kurudi Dodoma akitokea mkoani Iringa ambapo pamoja na kuhudhuria sherehe za Mei Mosi alihudhuria pia ufunguzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo.
Ilimlazimu Waziri Jafo kufanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo, ili aweze kujionea miundombinu mbalimbali katika shule hiyo iliyo anzishwa toka mwaka 1967.
Akizungumza na walimu, watumishi wasio walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kujionea hali ya miundombinu ya shule hiyo, Mhe. Jafo alieleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule kongwe zilizo kwenye mpango wa ukarabati mkubwa ili kuwa na mazingira bora ya kusoma na kujifunzia.
“Katika mwaka wa fedha wa 2017/18 tulikarabati shule kongwe 43 na katika mwaka huu wa 2018/19, shule hii pamoja na zingine kongwe 45 hapa nchini zitakuwa katika mpango kamambe wa kukarabatiwa kama tulivyokwisha fanya kwenye shule kama 43 za awali ambapo shule 89 zote kongwe tuwe tumezimaliza” alisema Waziri Jafo.
Aliongeza kuwa shule ya Wasichana Iringa imekuwa ni moja ya shule bora na hivyo kufanya wanafunzi wengi kupenda kuhamia kwenye shule hiyo.
Sambamba na ukarabati huo Mhe. Jafo ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zote ambazo ziliainishwa mbele yake ikiwepo upungufu wa walimu wa Fizikia na Hisabati pamoja na stahiki za walimu.
“Mama yetu Nkondola amewasilisha changamoto za walimu wa Hesabu na Fizikia lakini pia maslahi ya walimu, naomba nieleze kuwa suala hilo nimelichukua lakini niwaahidi kutuma wataalam kutoka kwenye wizara yangu pamoja na wizara nyingine za kisekta kuja kufanya tathmini ya kina juu ya haya mliyoniambia,” alisema waziri Jafo.
Aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii huku akitoa ahadi  kwa jumuiya hiyo kuwa endapo katika mitihani yao ya mwisho ya kidato cha sita watapata daraja la kwanza (DV.1) zaidi wanafunzi ya 30 atawandalia sherehe ndogo ya kujipongeza na wale watakaopata daraja la kwanza kati ya pointi 3-5 wataalikwa bungeni kwa gharama zake yeye Mhe.Jafo.
Mhe. Jafo akiwa katika ziara hiyo, alikagua miundombinu ya shule ikiwapo Mabweni, Vyoo, Bwalo la Chakula, Jiko na Ofisi za Walimu na kisha kufanya mazungumzo na walimu, watumishi wasio walimu wanafunzi sambamba na wananchi wanaozunguka eneo la shule hiyo.

Huo umekuwa ni utamaduni wa kiongozi huyo mwenye dhamana na OR TAMISEMI kila anapopata fursa kutembelea mikoani kutembelea shughuli za maendeleo kwa wananchi na sekta zote ili kujionea maendeleo ya watu na shughuli zao.


Anaandika Atley Kuni- OR TAMISEMI

Matangazo

  • Badili Tahasusi kwa Wanafunzi Kidato cha Tano Tarajali na Vyuo vya Kati March 29, 2021
  • Kitabu cha Maombolezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. John Pombe Joseph Magufuli March 18, 2021
  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TARURA Iringa watumia shilingi milioni 153 kukarabati barabara za Kalenga

    April 12, 2021
  • Shilingi bilioni 1.5 zatumika kujenga vituo vinne vya afya Tunduru

    April 12, 2021
  • Waziri Ummy aanza na Sekretarieti za Mikoa

    April 12, 2021
  • Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais TAMISEMI akabidhiwa ofisi

    April 12, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.