• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Serikali Yaagiza Halmashauri 30 Kuhamia na Kujenga Miundombinu

Imewekwa tar.: February 11th, 2020

Serikali imeagiza Halmashauri 30 zilizotakiwa kuhamia katika makao yao ya kiutawala kujenga ofisi za utawala na kuzikamilisha kwa wakati ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akitoa agizo hilo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga wakati wa ziara yake wilayani Geita ambapo aliongea na watumishi na kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo ameziagiza halmashauri 30 kuwa pamoja na kuitikia wito wa Mheshimiwa Rais Magufuli kuhamisha makao yao ya Halmashauri tangu Novemba 7, 2019 bado kuna changamoto ya mvutano wa kimaamuzi ni wapi makao makuu ya halmashauri yajengwe na hili linachelewesha huduma kwa wananchi.

“hakikisheni taratibu za eneo lililopendekezwa ujenzi wake unaanza mara moja ili muhamie kwa wakati hii ni pamoja na halmashauri nyingine 29 ambazo Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza tangu tarehe 7 Novemba, 2019”

Mhandisi Nyamhanga amesema pamoja na halmashauri hizo 30 kutii agizo la Mhe Rais Magufuli, halmashauri nyingi bado zimepanga kwenye majengo binafsi na wengine wapo katika ofisi za kata, shule, vituo vya afya, hospitali na majengo mengine kama magala ya chakula na kwamba hii haikubaliki kwani kuna baadhi ya halmashauri ambazo bado zina malumbano ya wapi majengo hayo ya utawala yajengwa.

Amesema agizo hilo ni la mara moja kwa halmashauri kuanza ujenzi na kukamilisha kwa wakati ili wananchi wafaidi matunda ya kupata huduma bora, karibu na kwa wakati lakini pia kutambua mipaka mipya ya kiutawala kwenye vitongoji, vijiji na wilaya ili kuandika hati za halmashauri.

Mhandisi Nyamhanga amezitaja baadhi ya halmashauri ambazo zimemaliza mchakato wa kutambua maeneo yao ya utawala na kuanza mchakato wa hati za halmashauri ambazo ni muhimu pia kwa ajili ya uchguzi mkuu wa 2020 kuwa ni pamoja na halmashauri za wilaya ya Mbulu (Manyara), Kibaha (Pwani), Handeni (Tanga), Uyui (Tabora) na Tanganyika (Katavi).

Wakati wa ziara hiyo Nyamhanga amekagua kituo cha afya Nzela ambacho kimepatiwa shilingi milioni 500 kwa ajili ya vifaa tiba na ukamilishaji wa majengo mengine ili kukipandisha hadhi kuwa hospitali ya wilaya ya Geita.

Mbunge wa Geita Joseph Musukuma ameomba kurejeshwa kwa shilingi milioni 293 ambazo zilirudishwa hazina kwenye mfuko mkuu wa Serikali baada ya kuvuka mwaka ili kumalizia baadhi ya kazi zilizobaki katika hospitali hiyo teule ya wilaya.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa Geita Dennis Bandisa amesema halmashauri ya wilaya ya Geita ina watu wapatao laki 9 lakini kimapato inazidiwa na halmashauri ya Mji Geita lakini pia kuna changamoto ya kiutawala katika Mji mdogo wa Geita ambapo Mtendaji wa kijiji ndiye anayefanya kazi kama Mkurugenzi wa Mji mdogo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashuri ya Wilaya ya Geita Bw. Ally Kidwaha amesema tayari wamepata eneo la ekari 400 kwa kushirikiana na Wadau wengine kujenga ofisi za halmashauri ya wilaya na kupima viwanja ili kuboresha makao ya halmashauri hiyo.

                      Anaandika Fred Kibano


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.