• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Serikali, wadau wa maendeleo wajadili mikakati ya kuzuia maambukizi ya malaria

Imewekwa tar.: May 10th, 2019

Na Mathew Kwembe

Serikali imesema kuwa ili kukabiliana ipasavyo na maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini wadau wa maendeleo wanapaswa kushirikiana na serikali katika kutafuta raslimali fedha zitakazosaidia kuzuia mbu wanaoeneza malaria ndani na nje ya kaya.

Akifungua kikao cha siku moja baina ya serikali na wadau wa maendeleo wanaofadhili mpango wa kuzuia malaria nchini mjini Dodoma leo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima amesema ili nchi ifanikiwe katika vita dhidi ya mbu wanaoambukiza ugonjwa wa malaria hakuna budi kuwekeza katika kutafuta raslimali zitakazowezesha kutekeleza mpango wa kuua mazalia ya mbu.

Amesema utokomezaji wa mazalia ya mbu ni mpango wa serikali ya awamu ya tano na tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli amekwishaagiza kuwa dawa zinazotengenezwa katika kiwanda cha kuua wadudu kilichopo kibaha mkoani Pwani zinunuliwe na zisambazwe katika halmashauri zote 184 na mikoa 26.

“Changamoto iliyopo ni kuwezeshs raslimali stahiki kwa ajili ya kuwezesha kutekeleza mpango huu katika maeneo yote nchini,” amesema.

Kwa mujibu wa Dkt Gwajima ili kuweza kutekeleza mpango wa kutokomeza mazalia ya mbu nchi nzima kutahitajika fedha, pump za kupuliza dawa hizo kwenye mazalia na wataalamu wa kunyunyiza dawa hizo kwa ufanisi.

Amesema pamoja na kuwepo kwa juhudi za kuhakikisha kuwa kila kaya inatumia vyandarua vyenye dawa ili kukabiliana na mbu wakati wa kulala lakini serikali ya awamu ya tano imeweka kipaumbele cha kuhakikisha kuwa mazalia ya mbu yanatokomezwa katika mikoa yote 26 na halmashauri 184 nchini ili ifikapo mwaka 2020 na juhudi hizi zilenge kuwezesha kiwango cha maambukizo ya malaria kufikia chini ya asilimia 1 kutoka asilimia 7.3 hivi sasa.

Amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakishambuliwa na mbu wakiwa nje ya nyumba zao hivyo hapana budi kuhakikisha kuwa mazalia ya mbu yanawekewa dawa walau mara moja kwa wiki ili kutokomeza wadudu hao wasiendelee kuzaliana na hivyo kuongeza kiwango cha maambukizo.

“Tayari serikali imekwishajenga kiwanda cha kutengeneza dawa za kuua mazalia ya mbu kilichopo Kibaha mkoani Pwani, hivyo ni matarajio yetu kuwa, juhudi za sasa zielekezwe katika kutafuta fedha kwa ajili ya kununua dawa hizo, pump za kunyunyizia pamoja na gharama za kuwezesha wataalam kutekeleza kazi hiyo,” amesema.

Kwa upande wake Meneja programu ya mpango wa taifa wa kuzuia Malaria Dkt Ally Mohamed amesema kuwa ili kuweza kutekeleza mpango huo kikamilifu wataalamu wa kunyunyiza dawa ya kuua mazalia ya mbu watapaswa kuifanya kazi hiyo kila wiki.

“Tunatarajia kila kata moja walau iweze kupata walau pump mbili za kunyunyizia dawa,” amesema.

Dkt Mohamed ameongeza kuwa tofauti na ilivyokuwa kabla sasa mbu wanauma zaidi nje ya nyumba kuliko ndani ya nyumba hali inayofanya serikali ya awamu ya tano kuweka msisitizo kwenye mbinu hii ya kuyatambua na kuyawekea mikakati ya kutokomeza mazalia ya mbu kama njia mojawapo ya kukabiliana na maambukizi ya malaria.

Naye Afisa msimamizi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya Malaria Bwana Wilfred Mwafongo amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 77.7 ya mbu jike wanaambukiza ugonjwa wa malaria ndani na nje ya nyumba.

Hivyo bwana Mwafongo akataka juhudi za makusudi zifanyike katika kuhakikisha kuwa vita dhidi ya maambukizi ya mbu ifanyike ndani na nje ya nyumba ambapo ndani vitumike vyandarua vyenye viuatilifu na nje kuwepo na mpango wa kuua mazalia ya mbu kwa kunyunyiza dawa.

Awali Mratibu wa Malaria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bibi Stella Kajange amesema kuwa lengo la serikali ni kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kitaifa kutoka wastani wa asilimia 10 % kwa mwaka 2012 hadi chini ya asilimia 1% ifikapo Disemba 2020.

Dkt Gwajima amehitimisha kwa kutoa maelekezo kuwa, wataalamu wachanganue gharama zote za kuwezesha mpango huu ili, kila mdau apewe na achangie kwenye mpango huu kuendeleza pale tulipofikia sasa. Amesema, kikao cha Juni, 2019 kije na majibu ya utekelezaji.

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.