• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Sekta zatakiwa kushiriki kupunguza magonjwa yasiyoambukizwa

Imewekwa tar.: January 19th, 2019

Sekta zote nchini zatakiwa kushiriki katika kudhibiti magonjwa yasiyoambukizwa ili kuisaidia jamii katika kujiepusha na madhara makubwa yanayojitokeza   na kupunguza gharama kubwa zinazotumika kwa matibabu.

Hayo yamesemwa na wadau wa afya wanaojishughulisha na magonjwa yasiyoambukizwa kwenye Kikao  cha  tathmini  ya utekelezaji wa mpango Mkakati wa mwaka 2015/2020 wa udhibiti wa magonjwa yasiyoambukizwa  na kutoa  mwelekeo wa nini kifanyike  kwa sasa na baadaye kiichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa , Jijini Dodoma

 Wakichangia mada ya nini kifanyike kupunguza magonjwa yasiyoambukizwa wadau hao wamesema Serikali  inajukumu ya kuhakikisha huduma  za afya  zinaboreshwa kwa kujenga miundombinu ya msingi, kufanya utambuzi wa haraka wa magonjwa  na  kutoa tiba kwa wakati kwa  jamii  ili kudhibiti  magonjwa hao.

Akifafanua zaidi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.  James Kiolowe amesema kuna haja ya kushirikisha Sekta mbalimbali katika kupunguza changamoto mbalimbali zinazosababisha magonjwa yasiyoambukizwa nchini ili kila mmoja awe na jukumu la kulinda afya za jamii nchini.

“Umefika wakati Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuwa wao ni watunga sera washirikishe Wizara nyingine kama Kilimo, ardhi, Mazingira ili kuhakikisha wanahusika katika kutatua changamoto za afua za afya na kupunguza magonjwa yasiyoambukizwa nchini “Anasema Kiolowe

Wakati Huohuo Dkt. Msafiri Kabulwa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ameitaka jamii kushirikishwa kwa kina juu ya madhara yatokanayo na magonjwa yasiyoambukizwa nchini ili kupunguza vifo vya vijana na watoto ambao wengi wamekuwa wakiadhirika na magonjwa hayo.

“Ufike wakati jamii ishirikishwe kikamilifu katika kuhakikisha wanadhibiti magonjwa ili kupunguza vifo kwa jamii. kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba ” Anafafanua Kabulwa

Naye Katibu wa Chama cha Kisukari Tanzania Prof.Kaushik Ramaiya   amesema kuwa upo umuhimu wa jamii kupatiwa elimu juu ya madhara yatokanayo na magonjwa yasiyoambukizwa, hii itasaidia kupunguza vifo na gharama ya matibabu kwa jamii.

“Wananchi wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika kutafuta matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza wakati elimu ndio msingi wa kuwasaidia kujikinga na Maradhi mfano jamii inatumia gharama kubwa sana kumtibu mgonjwa mwenye kisukari kuliko kuzuia ugonjwa huo.”Anafafanua Profesa Kaushik

Aidha Rais wa Chama cha madaktari wa meno Tanzania Dkt. Ambige Mwakatobe amesema kunaumuhimu wa jamii kuhakikisha wanafuata ulaji wa vyakula  vinavyofaa ili kupunguza magonjwa yasiyoambukizwa kama vile kisukari na kansa.





Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.