• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Rais Magufuli Awataka Maofisa Tarafa kuzitunza Pikipiki alizowakabidhi

Imewekwa tar.: June 11th, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amewataka Maofisa Tarafa Nchini kuzitunza pikipiki 448 alizowakabidhi mapema leo hii kwa lengo la kuwahudumia wananchi.

Kauli hiyo ameitoa  leo hii alipokua kwenye hafla ya uzinduzi wa  jengo la TARURA Makao Makuu sambamba na kukabidhi pikipiki 488 za Maofisa Tarafa.

"Niwatake Maofisa Tarafa wote Nchini, mkazitunze pikipiki hizi,na sio kupakizana Mishikaki au kuzitumia kwa matumizi yasiyofaa, hata kama wewe Ofisa ni mwanamke usiiache hiyo pikipiki tafuta msaidizi wako akuendeshe na uweze kufanya kazi za umma kwa ufanisi". amesisitiza Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameelekeza Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuweka utaratibu wa kuaandikisha maofisa tarafa hao kipindi watakapokabidhiwa  pikipiki hizo ili kuweza kuwa na ushahidi pale kutakapo tokea uharibifu wowote katika pikipiki hizo au kuipoteza basi muhusika anatakiwa kuwajibika juu ya uharibifu huo ikiwa ni pamoja na kuilipa endapo itakua ameipoteza.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewapongeza watendaji wa TARURA kwa kukamilisha ujenzi wa jengo lao na kuwataka kutumia fedha zinazoletwa na Serikali kutekeleza miradi ya barabara za mjini na vijiji kwa ufanisi.

Rais Magufuli amesema Tanzania imepata fedha za msamaha kutoka  Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa kuidhinisha Dola 14.3 milioni za msamaha wa madeni kwa Nchi ya Tanzania kwa kuwa Nchi yetu imeweza kupambana vizuri na ugonjwa wa corona.

“Nitamuandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa IMF kwa niaba ya Watanzania kumshukuru,fedha za IMF tutazitumia kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona, na maendeleo mengine yatakayosaidia corona isirudi tena katika nchi yetu” ameweka wazi Rais Magufuli.

Aidha Rais  Magufuli ameongeza kuwa  tukitengeneza barabara nzuri watu wakapita haraka, hata mdudu wa corona hawezi kumsogelea yule anayekimbia, Corona bado haijaisha lakini imepungua sana hivyo tuendelee kuchukua tahadhari na Mungu wetu anatupenda na tuendelee kumtegemea yeye.

"Tunamshukuru sana Mungu kwa kutuepusha na ugonjwa wa Corona, mambo yanaenda vizuri na tusidharau dawa za kienyeji uchawi tu ndiyo mbaya, Nimetoa maelekezo kwenye Wizara ya Afya, kile kitengo cha madawa ya asili kiendelezwe kwa nguvu zote na bajeti yake iongezwe " ameeleza Rais Magufuli

Awali  Rais Magufuli aliwataka  wananchi wote waliohudhuria hafla hiyo  kutoa heshima ya kuwaombea aliyekuwa Rais wa Burundi Mhe. Piere Nkurunziza aliyetutoka siku chache zilizopita pamoja na Watu Nane waliofariki Dunia baada ya hiace waliyokua wamepanda kugongwa na Lori huko Mkoani Mwanza.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo amesema  takribani bilioni 89.1 ni fedha iliyotengwa kwa ajiri ya kukamilisha mtandao wa barabara za lami kilomita 51.2 katika mji wa kiserikali.

“Mhe. Rais, nikuhakikishie kuwa barabara hizo ulizoziwekea jiwe la msingi leo zitapambwa na miti ya matunda pembeni na taa zaidi ya 700 za barabarani ili kuleta hadhi katika Jiji la Dodoma kuwa makoa makuu ya nchi yetu,” amesema Mhe. Jafo.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo Mkurugenzi Mtendaji wa TARURA Mhandisi Victor Seif amesema jengo hilo lina sakafu(Flow) 3 na  limejengwa kwa kutumia mfumo wa Force Account na umegharimu takribani shilingi Bil 1.9.

Awali kabla ya hafla hiyo Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara za lami a mzunguko zenye urefu wa kilomita 51.2 katika mji wa Serikali Mtumba zinazojengwa na kusimiwa na TARURA.

MWISHO


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Waziri Jafo ataka Shilingi Bilioni 245 za Miradi ya Maendeleo zitumike kwa wakati

    March 01, 2021
  • Serikali yalegeza masharti mikopo ya asilimia 10

    February 27, 2021
  • Vikundi 23 Wilayani Busega vimenufaika na mikopo ya asilimia 10

    February 26, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.