• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Miradi ya TSCP yachochea uchumi Jiji la Mbeya

Imewekwa tar.: May 10th, 2019

Zaidi ya shilingi bilioni 14 zatumika katika ujenzi wa miundombinu ya barabara  na utengenezaji wa mitaro ya maji ya mvua katika Jiji la Mbeya jambo ambalo limesababisha uboreshaji wa mazingira na kuchochea uchumi wa Jiji  hilo.

Hayo yamesemwa na  Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya na Mratibu wa Mradi wa Uimarishaji Miji (TSCP) Bw. Osward Kasambala wakati akitoa maelezo juu ya maendeleo ya Mradi huo kwa timu ya ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) iliyotembelea jiji hilo kwa lengo la kukagua maendeleo ya miradi iliyo chini ya  mradi wa uimarishaji Miji  Tanzania(TSCP)

Bw. Kasambala amesema Mradi wa Uimarishaji Miji Tanzania umesaidia ujenzi wa Miundombinu katika Jiji la Mbeya kwa kuboresha mazingira, kuongeza kasi ya uchumi, kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuongeza Mapato ya Halmashauri ya Jiji hilo.

“Awali miundombinu ya Barabara katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya ilikuwa ni vumbi lakini kwa sasa baada ya Mradi wa TSCP kujenga miundombinu hali imekuwa tofauti kwani miundombinu imebadilika na kuwa kivutio kwa wananchi kukuza uchumi wa Jiji la Mbeya” Anafafanua Kasambala

Amesema mara baada ujenzi wa miundombinu ya barabara Halmashauri ya Jiji la Mbeya imeweza kuchochea hali ya uchumi na kuweza kuongeza mapato kutokana na wananchi wengi kuwekeza kwenye maeneo ambayo barabara zimejengwa ukilinganisha na awali ambapo barabara nyingi zilikuwa za vumbi.

Bw. Kasambala amezitaja barabara zilizojengwa chini ya Mradi wa Uimarishaji Mji (Tanzania Strategic Cities – TSCP) katika kipindi cha mwaka 2018/2019  kuwa ni barabara ya MUST yenye urefu wa kilometa 2.7,  barabara  kutoka Ilomba hadi Ivumwe yenye urefu wa kilometa 1.8 na ujenzi wa  Mtaro wa maji ya mvua  wenye urefu wa kilometa 2.8.

Wakati huohuo Bi Debora Mkemwa kutoka Ofisi ya Rais Tawala zaMikoa na Serikali za Mitaa ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa usimamizi wa ujenzi wa miundombinu hiyo na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa wakati na kuzingatia ubora na dhamani ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya mradi huo

Aidha  Jiji la Mbeya ni miongoni mwa majiji 5 na Halmashauri 3 ambazo zinanufaika na Mradi wa  uimarishaji wa miji unaosimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kufadhiliwa na Benki ya Dunia.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI MBEYA

Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.