• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Book History
    • Kuhusu Wizara
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Utawala
    • Directory
    • Vitengo
    • Muundo wa Wizara
    • Mikoa, Wilaya na Halmashauri
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji

Mhandisi Nyamhanga ataka Halmashauri zijibu na kufanyia kazi mapendekezo ya CAG

Imewekwa tar.: March 26th, 2019

Na Mathew Kwembe, Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa hoja zote zilizoibuliwa kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinajibiwa na kufanyiwa kazi mapendekezo ya wakaguzi kwa kuanzia na wakaguzi wa ndani.

Akizungumza kwenye kikao kazi cha upokeaji na uhakiki wa taarifa za majibu na mipango kazi ya utekelezaji wa hoja na mapendekezo ya CAG kwa hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa za mwaka 2017/18 leo katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo jijini Dodoma, Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa ni muhimu hoja zote zikafanyiwa kazi haraka na kwa ufasaha ili kunusuru upotevu wa fedha, kuboresha utendaji na kuimarisha utawala bora, jambo ambalo ndio msingi wa ukaguzi.

Amesema kuwa ni vema kila Mtumishi afanye kazi kwa kuzingatia sheria, Kanuni, Miongozo, Taratibu na kuwajibika bila kuoneana haya.

“Tukifanya hivyo, hoja zisizo za lazima zitaondoka na hata wakaguzi hawatatumia muda mwingi katika kufuatilia mambo ya msingi zaidi katika kuboresha utendaji,” amesema.

Kauli ya Katibu Mkuu Nyamhanga inafuatia kukamilika kwa zoezi la kujibu hoja za CAG lililofanywa na Wakurugenzi wa Halmashauri, Waweka hazina na Wakaguzi wa Ndani kutoka Halmashauri zote 185, zoezi lililoanza tarehe 19 na kukamilika tarehe 26 machi, 2019.

Mhandisi Nyamhanga ameongeza kuwa katika kujibu hoja za CAG na kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa maagizo ya CAG ya Hesabu za mwaka 2016/17 imeonekana kuwa kufikia mwezi januari 2019, jumla ya hoja asilimia arobaini na saba (47%) zilifungwa wakati asilimia 53% zilikuwa bado hazijajibiwa.

Katibu Mkuu amesema kuwa zoezi hilo liliendelea katika ukaguzi wa Hesabu za Mwaka 2017/2018 ambapo hali halisi ya utekelezaji wa maagizo ya CAG zitaonekana baada ya taarifa hiyo kuwasilishwa bungeni mwaka 2019.

Aidha Katibu Mkuu amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa hoja na mapendekezo ya taarifa ya CAG wanayafanyia kazi ili kuboresha utendaji wa kazi na kuimarisha uwajibikaji hali ambayo itawahakikishia wananchi na umma kwa ujumla matumizi mazuri ya fedha zao, na utendaji wenye ufanisi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunatekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kufanyia kazi maagizo ya CAG na kuchukua hatua stahiki kwa Watumishi,” amesema Mhandisi Nyamhanga na kuongeza:

“Ninaelekeza kuwa, Watendaji wakaendelee kufanyia kazi hoja na mapendekezo ya CAG na kuwasilisha kwa wakaguzi wa CAG.”

Katibu Mkuu amewaambia wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa mara tu baada ya taarifa ya CAG kuwasilishwa bungeno majibu na vielelezo viwasilishwe kwa wakaguzi wa CAG ndani ya siku 21 kwa mujibu wa sheria ambapo amesema kuwa hategemei kuona majibu ya awali yasiyojitosheleza ilihali watendaji hao walikutana jijini Dodoma kwa ajili ya kuyaboresha majibu hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi na Ufuatiliaji wa fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa Bi Miriam Mmbaga amesema kuwa kikao hicho kimefanyika kuanzia tarehe 19-26 Machi, 2019 ambapo kimewahusisha Wakurugenzi, Waweka Hazina na Wakaguzi wa Ndani kutoka Mikoa 26 na Halmashauri zote 185 nchini.

Amesema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuwawezesha Watendaji hao kujibu hoja za CAG, kuongeza uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi ili hoja hizo zisijitokeze tena katika halmashauri zao.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba akiongea kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri amesema kuwa halmashauri zimekuwa zikikabiliana na changamoto mbalimbali katika kujibu hoja za ukaguzi kwani hoja nyingine hasa zile za kisera zilipaswa kujibiwa na Wizara husika badala ya ilivyo sasa kujibiwa na halmashauri.

Pia amewaasa wakurugenzi wenzake wa halmashauri kuwapa ushirikiano wakaguzi wa ndani wa halmashauri zao pindi wanapohitaji magari kwa ajili ya kwenda kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri zao.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 TANZANIA BARA December 06, 2019
  • TANGAZO LA KUWAREJESHA WAGOMBEA WASIO NA MAKOSA YA KIKANUNI KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019 November 10, 2019
  • MAELEZO KUHUSU ZOEZI LA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU ZA MAOMBI YA UTEUZI WA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI October 30, 2019
  • TANGAZO NA ORODHA YA WALIOITWA AJIRA ZA MKATABA TAASISI YA BENJAMIN MKAPA October 25, 2019
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA YA AFYA REPLACEMENT October 25, 2019
  • Orodha ya Majina ya watumishi wa Ajira Mpya kada ya Afya September 18, 2019
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Jafo atangaza waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza, 2020

    December 05, 2019
  • Jafo ambana Mkandarasi SKOIL Building Contractors Limited

    December 04, 2019
  • Jafo akagua ujenzi wa hospitali ya Uhuru

    December 04, 2019
  • Halmashauri zapigwa marufuku kukopa Benki

    November 29, 2019
  • Angalia zote

Video

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Dodoma
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.