• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Mhandisi Iyombe atunukiwa Tuzo ya Utumishi Uliotukuka

Imewekwa tar.: December 4th, 2018

Shirika la maendeleo la Japan(JICA) limemtunuku Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandishi Musa Iyombe Tuzo ya Umahiri na Utumishi Uliotukuka.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania Toshio Nagase amesema amekabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Rais wa Shirika hilo na tuzo hiyo ni ya 14 ambayo hutolewa na Rais wa shirika hilo kwa pamoja na tuzo wanazo toa kwa watu binafsi na mashirika.

Ameongeza kuwa  Mhandisi Iyombe anaingia  miongoni mwa watu na mashirika 49 waliopatiwa tuzo za shirika hilo lengo ikiwa ni kuwatambua watu binafsi au Taasisi zinatoa mchango wa kipekee na kugusa maisha ya watu  katika kuboresha miundombinu, kuendeleza rasilimali watu, kuboresha maisha ya watu pamoja na kupunguza umasikini katika nchi zinazoendelea.

“Mhandishi Iyombe amefanya yote yanayostahili  kupata Tuzo hii tangu wakati akiwa anahudumia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kisha kuhudumu katika Wizara ya Ujenzi na ndipo kuja hapa OR-TAMISEMI na kote huko alikopita ametoa mchango mkubwa sana katika kuleta maendeleo kwa mtanzania na Taifa kwa ujumla” alisema Nagase.

Aliongeza kuwa mchango wa Iyombe ulianza kuonekana tangu mwaka 1984 mara tu alipomaliza shahada yake ya kwanza ya Uhandishi huko India na kufanya mafunzo kwa vitendo chini ya wataalamu wa Japan waliokua wanajenga barabara ya Kibiti – Lindi.

Kwa kipindi chote cha miaka 34 sasa amejitoa kwa moyo kutumia Taaluma yake ya Uhandishi kushiriki kuhudumu katika miradi mbalimbali ya maendeleo ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania ambayo mingine ilikuwa inasimamiwa na wataalm kutoka Japan.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watumishi kufuata nyendo za Mhandisi Iyombe za kuwatumikia wananchi kwa moyo ili waweze kuacha  alama ‘Legacy’ katika Utumishi wao wa Umma.

“Tuzo hii anayokabidhiwa Katibu Mkuu wetu leo asingeweza kuipata kama asingekuwa mahiri katika utendaji kazi wake na kujitoa kwa dhati kutatua kero za wananchi; Hii imepelekea yeye kuonekana kati ya wengi kuwa anastahili kutambulika kimataifa, Tuzo hii iwe somo kwetu tuweze kujifunza na kubadilika’ alisema Jafo.

“Nivigumu sana binadamu kumsifia au kuona mazuri ya binadamu mwenzake kama yuko hai lakini leo Mhandisi Iyombe una sifiwa ukiwa hai hii inaonyesha kuwa wewe ni kiongozi wa kuingwa kwani ni vigumu kutambua mazuri ya mtu akiwa hai” Alisema Jafo.

Naye Mhandisi Mussa Iyombe amesema kuwa tuzo hiyo sio yake bali ni tuzo ya watumishi wote kwani ushirikiano wao ndo umemfanya leo anapata tuzo hii kutoka kwa watu wa JICA.

“Siwezi sema tuzo hii ni yangu bali tuzo hii  ni yetu sote , nasema hivi kwani hapo nilipo bila ushirikiano wenu mimi ni singeweza kupata tuzo hii, kikubwa namshukuru Mungu na twendelee kumuomba Mungu ili tudumishe ushirikiano wetu katika utekelezaji wa wajibu tulio nao kwa watanzania” Alisema Iyombe.



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.