• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Makatibu Tawala Mikoa simamieni Matumizi na Manunuzi ya Umma katika Halmashauri

Imewekwa tar.: February 25th, 2019

Serikali imewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa na kusema itaendelea kuimarisha hali ya ukusanyaji wa mapato na kusimamia matumizi sahihi ya fedha za Umma kwenye halmashauri nchini ili kuinua uchumi wa mamlaka husika na kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha maboresho ya fedha katika halmashauri nchini ambapo amewataka Makatibu Tawala kusimamia ukusanyaji wa mapato ya halmashauri samabamba na matumizi ya fedha za Umma.

“tumewaita Makatibu Tawala wa Mikoa ili kuweza kuboresha hali ya masuala ya fedha katika mikoa na halmashauri zao ikiwa ni pamoja na mipango ya mikoa, vitu muhimu ni vya msisitizo ni matumizi ya fedha za Umma kuanzia fedha za makusanyo katika vyanzo vya halmashauri, kutoka Serikali Kuu na fedha za Wadau wa Maendeleo kwamba zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa”

Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa suala la kuimarisha Vitengo vya ukaguzi vya ndani limetiliwa mkazo ili kuweza kubaini ubadhilifu katika hatua za awali na pia kuimarisha Vitengo vya manunuzi ili kuona sheria, kanuni na taratibu za mwaka 2016 za manunuzi ya Umma zinafuatwa na kwamba Ofisi ya Rais TAMISEMI itafanya ukaguzi ili kubaini kama kuna ubadhilifu na ukiukwaji wa matumizi ya fedha za Umma.

Kwa upande wake Shomari Mukhandi Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Usimamizi wa Fedha Ofisi ya Rais TAMISEMI akitoa taarifa ya jumla ya mradi katika kikao tendaji cha mradi amesema kwa hivi sasa awamu ya tano inayokuja itahusisha mikoa yota ikiwa na malengo ya usimamizi wa matokeo mazuri ya fedha kwa kupata hati safi na kuboresha mapato ya halmashauri nchini.

“programu hii imechangia maboresho ya hali ya fedha katika hamashauri nchini ambapo asilimia 90 zisizo na mashaka zimeongezeka ikilinganishwa na asilimia sitini za hapo awali, aidha umewezesha kupanga na kusimamia mapato ya halmashauri kwani ongezeko la maptao ni asilimia 80 ya mipango yao ikilinganishwa na hapo awali”  

Naye Magreth Chipeta Afisa wa Serikali za Mitaa mkoa wa Rukwa amesema kimsingi  programu hii ya maboresho ya mfumo wa fedha imesaidia sana mkoa wa Rukwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ukilinganisha na ukusanyaji mdogo wa hapo awali ambapo imeongeza mapato kwa asilimia 30.

“awali mkoa wa Rukwa ulikuwa ukikusanya shilingi bilioni 2.1 mwaka 2012/2013 lakini mwaka 2017/2018 mfumo wa kielektroniki umesaidia kukusanya shilingi bilioni 6.9 sawa na ongezeko la asilimia 30, kwa mfano manispaa ya Rukwa pekee imekusanya asilimia 97 ya lengo walilojiwekea na Nkasi asilimia 82”

Aidha, Bi. Chipeta mfumo umesaidia kuondoa hoja za ukaguzi kutoka hoja 536 awali hadi hoja 282 kwa hivi sasa, mfumo pia umesaidia kutoa mafunzo kwa madiwani, watumishi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa na ofisi za halmashauri za wilaya mkoani Rukwa.  

Maboresho ya Programu ya Fedha (Public Financial Management Reform Programme - PFMRP) ilianzishwa hapa nchini katika mwaka wa fedha 2014/2015 na kukamilika mwaka 2016/2017 kwa lengo la kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa mapato na matumizi mazuri ya fedha za Umma ili kutoa huduma bora na kuleta maendeleo katika mikoa kumi ya Dodoma, Geita, Katavi, Mara, Simiyu, Mtwara, Njombe, Kigoma, Rukwa na Ruvuma ambayo ilikuwa nyuma kimapato.

Hivi sasa mfumo huu upo katika awamu ya tano na itakuwa ya miaka mitano kuanzia 2017/2018 hadi 2021/2022 na itahusisha mikoa yote ishirini na sita na unalenga uwazi, uwajibikaji, ufanisi na nidhamu katika matumizi ya rasilimali za Umma.

                                            Anaandika Fred Kibano




Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.