• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Kituo cha mabasi Mbezi Luis kutarajiwa kuanza kazi Oktoba, 2020

Imewekwa tar.: August 17th, 2020


Kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis kimefikia asilimia 77 ya ujenzi wake na kinatarajiwa kuanza kazi rasmi ifikapo Oktoba mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi  Joseph Nyamhanga anayetembelea miradi mbalimbali iliyopo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Jiji hilo Zipora Liana, amesema kukamilika kwa ujenzi huo kunatokana na juhudi za haraka zilizochukukiwa na Jiji pamoja na mkandarasi za kumaliza ujenzi kwa wakati.

Ujenzi huo ulioigharimu Serikali kiasi cha Shilingi Bilioni 50.9 pindi utakapokamilika utakifanya kituo hicho kuwa moja ya kituo bora kati ya vituo vya mabasi katika ukanda wa Afrika mashariki na kati huku kikitarajiwa kuchukua mabasi makubwa 108 kwa wakati mmoja.

Mbali na mabasi hayo, pia kitaweza kuchukua mabasi madogo zaidi ya mia moja huku kikiwa na huduma mbalimbali zikiwemo za migahawa, benki, zahanati kituo cha polisi, maduka pamoja na sehemu za kuoshea magari.

"Ujenzi wa kituo hiki ulipaswa kuwa umekamilika tangu Julai mwaka huu na kazi kuanza, changamoto mbalimbali zilizokuwa zimejitokeza ikiwemo mvua na ugonjwa Covid 19 ulisababisha kazi kuchelewa" amesema Liana.

Ameendelea kusema kuwa  mbali na hilo pia Jiji lilisitisha kuendelea na mkataba na aliyekuwa mkandarasi mshauri katika ujenzi huo ambaye kimsingi amesema kwa kiasi fulani alikuwa sehemu ya kuchelewesha kazi katika mradi huo kuweza kukamilika kwa wakati.

Bi. Liana amesema  matarajio ya kituo hicho kitaweza kukusanya kiasi cha  shilingi Bilioni 7.2 kwa mwezi zitakazotumika kwa ajili ya maendeleo mbalimbali ya Jiji hilo pamoja na taifa kwa ujumla.

Aidha akizungumza mara baada ya kupokea taarifa za ujenzi huo, Katibu Mkuu Ofisiya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga amesisitiza kukamilika mapema kwa ujenzi huo ili kuwezesha mabasi kuanza kutumia kituo hicho na kupisha  eneo la kituo cha sasa cha Ubungo ambapo kunatarajiwa kujengwa karakana ya mabasi yaendayo kasi.

Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa  malengo ya Serikali ni kuona mradi huo umekamilika mapema ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo kwa sasa katika kituo cha Ubungo na kusababisha kero kwa watumiaji wa kituo hicho huku akisisitiza kuwa matarajio ni kuona kituo hicho kinaanza kutumika katikati ya Oktoba mwaka huu.

Aidha amesisitiza kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi yake hivyo jambo la msingi ni kuona miradi hiyo ikitunzwa ili kuepusha kusababisha hasara ya fedha iliyotokana na fedha za wananchi.

Na. Angela Msimbira DAR-ES-SALAAM

Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.