• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Kamati ya Bunge ya Uganda Yamwagia Sifa Mradi wa DMDP

Imewekwa tar.: May 14th, 2018


Kamati ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kutoka Nchini Uganda (PAC-LG) imemwagia sifa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam unaoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Tano za Mkoa wa Dar es salaam.

Kamati hiyo yenye zaidi ya wajumbe kumi waliotemebelea Mradi wa DMDP unaotekelezwa chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wamesema ni mradi wa mfano na kuigwa na Nchi za Afrika Masshariki zinazopata mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia.

Akizungumza katika ziara hiyo ya mafunzo Mwenyekiti wa Kamati hiyo (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu amesema lengo la ziara yao ni kuona namna ambavyo miradi ya Uboreshaji Miundombinu inayotekelezwa kwa fedha za Mkopo toka Benki ya Dunia;

“Tunapenda kuona ubora wa miradi hiyo, taratibu za ulipaji fidia zilivyofuata, maelekezo ya mkopo wa fedha hizo yalivyozingatiwa na zaidi namna ambavyo fedha zilivyopokelewa, zinavyosimamiwa na wataalamu, zinavyotumika na zinafanyiwa ukaguzi na zaidi suala zima la thamani ya fedha”Value for Money” kuonekana katika miradi hiyo” alisema Mhe. Okumu.

Akipokea ujumbe huo toka Bunge la Uganda Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege amesema mradi huu umetekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu sasa na mafanikio yaliyopatikana ni makubwa na kwa kiasi kikubwa umesaidia kuwapunguzia kero wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam.

“Karibu mjifunze kwa kuona mtaona barabara zilivyojengwa kwa ubora wa hali ya juu, njia za bora waenda kwa miguu, mifereji yenye viwango ya kusafirishia maji ya mvua, masoko na ofisi za miradi pamoja na maabara za kisasa za kupima ubora wa barabara zinazoendelea kujengwa “ alisema Kandege.

Akielezea Miradi inayotekelezwa chini ya fedha za Mkopo wa Benki ya Dunia Mratibu wa Miradi hiyo toka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Eng. Davis Shemangale amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na unalengo  la kuboresha Jiji la Dar es salaam lizidi kuwa bora katika Sekta ya miundombinu, usafiri mjini pamoja na  usalama

Eng. Shemangale aliongeza  kuwa mradi huo pia utaboresha makazi bora sambamba na kujenga uwezo wa Kitaasisi pamoja na mifumo stahiki na ya kutosha kutunza kumbukumbu na takwimu  itakayosaidia katika Ukusanyaji wa mapato.

Naye mratibu wa mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (DMDP) Eng. Emmanuel Ndyamukama amesema Katika awamu ya kwanza ya mradi huu itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 300 ambazo ni Fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia. Aidha Shirika la maendeleo la Nchi za Nordic litatoa ruzuku ya dola za kimarekani Mil. Tano kwa ajili ya kukabili changamoto za mabadiliko ya Tabia ya Nchi na huku Serikali ya Tanzania ikichangia takribani Dola za Kimarekani  Mil. 25.3 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi  walioathirika na mradi.

Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa iko katika ziara ya mafunzo kwa muda wa siku Tano na itatemebela miradi ya uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (DMDP), Mabasi yaendayo haraka (BRT) kasha kuelekea katika Manispaa ya Morogoro ambako watatembelea mradi wa uboreshaji na uimarishaji wa Mamlaka za Miji (ULGSP) kasha kumalizia na Jiji la Dodoma ambako watajione mradi wa Uboreshaji Miji Kimkakati (TSCP).

Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Mweli awatega Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu kwenye Mfumo wa PREM/PREMS.

    January 10, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.