• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Kaaya awahimiza Vijana kujiajiri kupitia kilimo

Imewekwa tar.: October 16th, 2019

VIJANA wakiwamo wanafunzi wa sekondari wametakiwa kukitumia kituo cha kilimo, taaluma na mawasiliano kilichopo Mpwapwa Mkoani Dodoma kupata ujuzi wa kilimo cha mbogamboga na maua ili waweze kuondokana na tatizo la ajira.

Wito huo ulitolewa jana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Nchini (ALAT),  Elirehema Kaaya alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa kupitia Mradi wa kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC) inayotoekelezwa katika Halmashauri za Mikoa ya Dodoma na Kigoma kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  na Ubalozi wa Dernmark.

Kaaya amesema kuna haja ya wazazi ,walezi na walimu kupeleka Watoto wao katika kituo hicho cha kilimo ili waweze kujifunza na kujikwamua  kiuchumi mara baada ya kumaliza masomo yao  na kuleta maendeleo kwa jamii inayowazunguka.

 “Ni vyema kwa vijana wakiwemo wale waliokuwa sekondari kutumia kituo hiki kujifunza ili wanapomaliza masomo yao wakiwa wanasubiri matokeo basi watumie ujuzi kujishughulisha na kilimo na kama hawataendelea na masomo basi waendelee na hii itapunguza malalamiko ya kukosa ajira. Watanzania wanatakiwa kujua hakuna ajira inayozidi kilimo cha aina hii, hii elimu wanayopata hapa wakaifanye wakati wanasubiri matokeo ya kuendelea na elimu ya juu,”Amesema Kaaya.

Kaaya ameeleza uboreshaji wa kitua hicho umetumia zaidi ya Sh milioni 150 na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwawa milioni 90 kwa ajili ya kuandaa kitalu, kutoa mafunzo kwa nguvu kazi ambapo wakulima wamepata elimu hiyo.

Kaaya amesema kumekuwa na mwamko mdogo wa vijana kuchangamkia mafunzo yanayotolewa na kituo hicho na wengine kuona kama kilimo ni utumwa wakati kinaweza kuwakwamua kiuchumi.

Hata hivyo, Kaaya ameagiza kujengwa kwa mfumo wa kuvuna maji ya mvua kwenye majengo ya kituo hicho ili kukabiliana na upungufu wa maji kwenye eneo hilo na kutengeneza uzio wa asili kama michongoma.

“Nimejulishwa kuwapo kwa kutokuwa na maji ya kutosha, uzio na kutokuwa na nguvu kazi wakihitajika vibarua hawapatikani, lakini kunachangamoto zingine tunapaswa tuzibadili kuwa fursa, mfano tunaweza kujenga uzio wa michongoma na pia kuweka mifumo ya kuvuna maji,”Amesema.

Aidha, Kaaya ametoa wito kwa Halmashauri nchini, jamii na taasisi zikiwemo shule, hospitali na ofisi mbalimbali kuweka mifumo ya uvunaji maji ya mvua ambayi yatatumika kutumika kwa shughuli nyingine ikiwemo usafi na umwagiliaji.

Awali, akitoa taarifa ya kituo hicho, Mkuu kituo cha Kilimo, Taaluma na Mawasiliano Kibakwe, Samson German amesema kituo hicho kinatoa huduma za kilimo na mifugo kwa wakulima katika eneo husika.

Aidha, amesema mpaka sasa kituo kimetoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi 30 wa mafunzo ya ujuzi waliotoka chuo cha kilimo na mifugo Visele Mpwapwa, pia wakulima 60 kutoka vijiji vya Kibakwe, Iyenge na Chamtumile juu ya kanuni za kilimo bora cha mbogamboga ili kuboresha lishe na kuongeza kipato.

Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI



Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Tangazo la kazi kada ya Afya January 20, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Mweli awatega Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu kwenye Mfumo wa PREM/PREMS.

    January 10, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.