• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

Imewekwa tar.: March 3rd, 2021

Na Atley, DODOMA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo, ametoa siku 12 kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Dodoma kuhakikisha kero zilizopo katika Soko la Job Ndugai na Stendi ya mabasi ya Dodoma zinatatuliwa.

Jafo ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutembelea miradi minne ya kimkakati ambapo alionyesha wazi kutoridhishwa na miradi hiyo miwili kwa namna inavyoendeshwa.

Akiwa katika mradi wa Soko la Job Ndugai, Waziri Jafo alionesha kutoridhika na uongozi wa Soko hilo kuwatoza Wafanyabiashara  wenye vizimba kulipa ushuru wa shilingi 70,000 badala ya shilingi 20,000.

Kero nyingine aliyoishuhudia Waziri Jafo ni kitendo cha Malori makubwa ya mizigo kuendelea kushusha na kupakia katika soko la majengo na masoko mengine yaliyopo katikati ya jiji hali inayosababisha malori hayo kuharibu miundombinu ya barabara.

Kufuatia hali hiyo Waziri Jafo ameuagiza uongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa kuanzia tarehe 10 mwezi huu malori yote makubwa ya mizigo yanashusha na kupakia katika soko la Ndugai.

“Sijaridhishwa na hali ya soko hili nimekuwa Very Dissapointed, naagiza kabla ya tarehe 10 soko liwe ‘busy otherwise’ miradi yote tutakuwa tunapeleka Halmashauri nyingine maana wapo waliohitaji hawajapata lakini cha kushangaza hakuna kinachoendelea hapa,” amesema na kuongeza:

“Nikija tena hapa nikute mizigo inashushwa na magari madogo ya mizigo yachukulie hapa maana huko barabara zimeharibika wakati serikali imeweka maeneo maalum kwa ajili ya kushusha mizigo, Mimi siwaelewi kwa nini ushushaji mizigo Bado unaendelea katikati ya jiji,”amesema.

Waziri Jafo alisema inawezekana jiji hawajajipanga kwakuwa alitegemea akifika eneo hilo akute pamechangamka na malori yanashusha mizigo mikubwa na kwamba wangejipanga hali isingekuwa hivyo.

Kuhusu Stendi ya mabasi, Waziri huyo aliwapa siku mbili uongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha wanaweka Scanner na mashine za kukusanyia mapato za POSS kwa ajili ya  ukusanyaji mapato katika mageti yote na yawe yanafanya kazi ili kila mwananchi awe na uhuru wa kupita anapotaka.

“Viongozi wa mkoa huu nimeridhishwa na utaratibu wa mabasi yote kuingia stendi na abiria kupakiwa na kushushwa hapa lakini changamoto ya matumizi ya geti moja tu ifanyiwe kazi,  angalieni vizuri maana inawezekana kuna mtu maalum kapewa ikiwezekana muwe na vitambulisho,” amesema.

Amemtaka meneja wa stendi hiyo kutoa vitambulisho kwa mawakala wa mabasi wanaofanya shughuli Stendi ili kero ya Suma JKT ya kuwazuia kutumia mageti mengine imalizike

“Meneja wa Stendi na watendaji wengine simamieni askari wanaofanya kazi hapa ili kuondokana na changamoto ya watu kubambikiwa makosa ili watoe fedha maana inaashiria vitendo vya rushwa jambo ambapo sio zuri,” amesema.

Kuhusu mradi wa Chinangali Park ambao mwekezaji wake  aliyejulikana kwa jina la Captown analipa ushuru wa sh. Milioni 18 kwa mwezi alishauri mkataba wake kurekebishwa ikiwezekana uwe wa miaka mitatu badala ya mmoja ili akishindwa kufanya kazi vizuri apewe mtu mwingine.

“Badilisheni mkataba uwe wa miaka mitatu ukiisha kama hajafanya vizuri mchukue hatua maana muda wa mwaka mmoja ni mdogo na hatujui kama kwa muda huo mtu anaweza kuaminika na taasisi za kibenki kukopa, muongezeeni,”amesema.

Kwenye Mradi wa maegesho ya magari Nala, ambao malori zaidi ya 100 kwa sasa yanapaki Waziri Jafo alionyesha kuridhishwa na mradi huo huku akiagiza huduma za kibinadamu kuwekwa eneo hilo ili madereva wapate mahitaji maalum na wawekezaji wahamasishwe kuja kuwekeza.

Akitoa shukrani baada ya ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binillith Mahenge alimhakikishia Waziri Jafo kuwa changamoto zilizoainishwa na wafanyabiashara zitafanyiwa kazi na maelekezo yaliyotolewa yatatatuliwa ili jiji lipate faida na wananchi wapate huduma.

 



Matangazo

  • Badili Tahasusi kwa Wanafunzi Kidato cha Tano Tarajali na Vyuo vya Kati March 29, 2021
  • Kitabu cha Maombolezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. John Pombe Joseph Magufuli March 18, 2021
  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TARURA Iringa watumia shilingi milioni 153 kukarabati barabara za Kalenga

    April 12, 2021
  • Shilingi bilioni 1.5 zatumika kujenga vituo vinne vya afya Tunduru

    April 12, 2021
  • Waziri Ummy aanza na Sekretarieti za Mikoa

    April 12, 2021
  • Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais TAMISEMI akabidhiwa ofisi

    April 12, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.