• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

‘Jiimarisheni zaidi katika Uongozi na Utendaji’ Waziri Mkuu Majaliwa

Imewekwa tar.: December 3rd, 2018

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali kutumia fursa ya mafunzo wanayoyapata mara kwa mara  kujiimarisha zaidi katika Uongozi na Utendaji kazi wao wa kila siku.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo Jijini Dodoma alipokua akifungua mafunzo ya siku Tano kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa Tanzania bara yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi.

Alisema kuwa Mhe. Rais na sisi wasaidizi wake tuna imani kubwa na uongozi na utendaji kazi wenu, hatuna shaka yeyote maana mlipekuliwa sana wakati wa mchakato wa kuelekea uteuzi wenu, mkiwa kama wasimamizi wakuu  na watendaji wakuu wa shughuli zote za Serikali katika Mikoa yenu; huu ni wakati mzuri wa kujiimarisha zaidi katika uongozi na utendaji kazi wenu.

“Mada zilizochaguliwa ni muhimu na muafaka katika kuboresha Uongozi na Utendaji kazi  hivyo kila mmoja wenu ajithathmini kupitia mafunzo haya kisha aboreshe zaidi utendaji kazi wake ili tuweze kumhudumia vizuri mtanzania” Alisema Mhe. Majaliwa.

Aliongeza kuwa katika mada inayohusu Majukumu na Mipaka ya kazi  mtajifunza namna ya kufanya kazi bila mikwaruzano isiyo na tija baina yenu na viongozi wa mihimili mingine ya Dola, Viongozi wa Kisiasa na Watendaji wengine Serikalini.

Pia alibainisha kuwa katika mada ya Uongozi, Hisia na Mahusiano Mahala pa kazi kuwa Viongozi hao watafahamishwa  kwa undani mbinu za kuwaongoza watumishi walio chini yao kwa kujenga na kudumisha mshikamano na ushirikiano wa pamoja (Team work).

“Hii itawasaidia zaidi kuona namna mnavyotegemeana na watumishi wa kada na ngazi mbalimbali katika kutimiza majukumu yenu. Ni muhimu sana kufanya kazi kama timu moja ili muweze kuyafikia malengo ya Taasisi kwa upana wake na si malengo ya mtu au kiongozi mmoja” alisema Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa.

Kupitia mafunzo mtakayoyapata muyatumie kutafakari na kujithathmini kuhusu hatua za kujiimarisha zaidi kiungozi na kiutendaji. Hatua hizo ni lazima ziwe pamoja na kubadilika kwa mtazamo na kujirekebisha endapo mtabaini maeneo mliyokuwa mkikosea tangu mlipokabidhiwa Ofisi hadi sasa alimalizia Mhe. Majaliwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo alisema pamoja na changamoto bado zipo lakini kwa kiwango kikubwa baada ya mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa viongozi mbalimbali utendaji kazi umebadilika.

Waziri Jafo pia amewapongeza Wakuu hao wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa kwa Usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika maeneo yao.

“Nimeona katika miradi ya kimkakati inayotekelezwa sasa kama Ujenzi wa Vituo vya Afya ambao unaendelea Nchi Nzima mmefanya kazi nzuri, usimamizi wenu umeleta Tija kwani ujenzi wa vituo vya Afya umetekelezwa kwa ufanisi wa hali ya juu” Alisema Mhe. Jafo.

Akitoa Tathmini ya Ujenzi wa Viwanda ambavyo vimesimamiwa na Wakuu hao wa Mikoa  Mhe. Jafo amesema mpaka sasa Agenda hii imefanikiwa kwa asilimia 49.2 na mpaka sasa viwanda ambavyo vimekwishajengwa kwenye mikoa yetu ni 1280 kati ya 2600 alivyoagiza wakati anazindua kampeni ya Mkoa wangu Kiwanda Changu.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof.Joseph Semboja alisema mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini yamekamilika na yamepata mafanikio makubwa.

Pia Prof. Semboja aliwataka viongozi hao kujikita kwenye mafunzo wanayoyapata.

Alitaja malengo ya mafunzo hayo kuwa ni kuimarisha uwezo wa kufanya maamuzi ya kimkakati, kuimarisha uwezo wa kuongoza rasilimali watu na kusimamia nyingine na kujijengea sifa binafsi za uongozi.


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.