• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

JAFO: Wataalam fanyeni upya tathmini ya gharama za ujenzi Hospitali ya Uhuru.

Imewekwa tar.: September 13th, 2019

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amewataka wataalam wa ujenzi kutoka SUMA JKT na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kukaa chini na kutafakari namna ya kujenga hospitali ya Uhuru kwa gharama nafuu kulingana na fedha iliyopo sh bil 3.

Mhe Jafo ametoa maagizo hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo na kupokea taarifa kutoka kwa msanifu majengo kutoka Suma JKT Bw. Michael Gama wanaojenga hospitali hiyo na kusema gharama za ujenzi ni sh bil 6.1.

Amefafanua kuwa hospitali hiyo inajengwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Magufuli kutokana na mapenzi yake kwa wananchi hivyo kushindwa kuikamilisha ina maanisha watu na vyombo vya serikali vimeshindwa kuendeleza juhudi zake.

“Mimi niwaagize wataalam kakaeni chini mtafakari jinsi gani tutajenga hii hospitali itajengwa lakini kwa style hii haiwezekani, angalau tungekuwa hatuna fedha lakini fedha tunayo bil 3, hivyo tafakarini nini kifanyike jengo hili liweze kujengwa” Amesisitiza Mhe. Jafo.

Ameendelea kusema,  litakuwa jambo la ajabu kama Nyang,wale na Kyerwa walipata sh bil 1.5 ujenzi wa hospitali na zimekamilika halafu hapa ishindikane kwa sh bil 3 na wataalam wote wapo hapa jambo hilo haliwezekani.

“Na ndio maana nilitaka majengo haya yapewe vyombo vya serikali maana wao ndio wanajua maono na dhamira ya Rais wetu katika kuhakikisha inakuwepo hospitali ya Uhuru,sasa mimi nimejivua kama waziri wake kazi yangu nataka jengo hili likamilike kwa gharama ya shilingi bilioni 3.

Ameendelea kuhoji kuwa kazi imeanza lakini shida ni kwenye gharama za ujenzi hivyo ujenzi utaanza lakini hautakamilika wakati dhamira ya serikali ni wananchi wapate huduma bora za afya, natamani tungeweka majengo yetu ya kawaida lakini kwa hapa ni tofauti hivyo sina uhakika wa kukamilisha ujenzi wa Hospitali hiyo.

 Wakati huohuo msanifu majengo kutoka SUMA JKT wamekubali kukaa chini  na kuangalia gharama za ujenzi katika usanifu ili kufikia muafaka wa kuendelea na ujenzi hadi kukamilika kwa gharama iliyotolewa na Serikali.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo  Bw. Gama amesema ujenzi wa mradi huo ulianza agosti 16 na kwa sasa wamefikia hatua ya uchimbaji wa msingi na matarajio yakiwa kukamilisha uchimbaji huo septemba 16 mwaka huu.

Hata hivyo amesema bado hawajasaini mkataba bali wamesaini makubaliano ya awali na ndio hayo wanayotumia kufanyia kazi kwa kuwa wanaendelea na mapatano ya gharama ya ujenzi.

Kwa upande wake mhandisi kutoka Wakala wa Majengo (TBA) Bw. Elias Tillya amesema ili kuendana na kiasi cha fedha kilichopo inabidi kupunguza mita za mraba za jengo ambazo ni 4400 kwa sasa.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw.  Athuman Masasi amesema hawakuridhishwa na gharama ya ujenzi ya shilingi bil 6 hivyo tayari walishafanya mazungumzo  na wataalam kuona haja ya kukaa pamoja na kuliona hilo.

“kwa mujibu wa utaratibu wa kisheria waliouweka ilikuwa tufanye negosition kati ya halmashauri na wao,sasa tulichoshauriana tukasema hebu fedha tulizotoa mil 900 kazi ifanyike ili tuone itaishia wapi wakati maelewano ya bei inaendelea,na ndio maana hatujafunga nao mkataba” Amesisitiza Bw. Masasi.

Aidha hospitali hiyo inajengwa baada ya Rais Magufuli kufuta sherehe za Uhuru mwaka jana na fedha zake kiasi cha sh bil 1.5 kuelekezwa kwenye ujenzi huo na kuongeza sh bil 1.5 nyingine zilizotokana na gawio la kampuni ya simu ya Airtel.

Na. Angela Msimbira CHAMWINO

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Waziri Jafo ataka Shilingi Bilioni 245 za Miradi ya Maendeleo zitumike kwa wakati

    March 01, 2021
  • Serikali yalegeza masharti mikopo ya asilimia 10

    February 27, 2021
  • Vikundi 23 Wilayani Busega vimenufaika na mikopo ya asilimia 10

    February 26, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.