• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Jafo aziagiza Halmashauri zote nchini kuwa wabunifu wa miradi ya Maendeleo

Imewekwa tar.: August 27th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaweka mikakati kwa kubuni miradi ambayo itawasaidia katika kujiwekea vitega uchumi na kukuza mapato katika Halmashauri zao ili kuachana na utegemezi katika Serikali.

Ameyasema hayo leo wakati wa utiaji wa saini Miradi ya Ujenzi wa majengo mawili ya vitega uchumi vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square, Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema Halmashauri zote nchini zinatakiwa kuwa wabunifu, kujipanga na kuweka mikakati ya kuondokana na unyafuzi wa mapato kwa kuanzisha miradi ambayo itasaidia kuongeza mapato na kuleta maendeleo kwa jamii.

Amesema kuwa kama Halmashauri zote zingekuwa wabunifu na kuamua  kujitoa katika utendaji kazi kusingekuwa  na unyafuzi wa mapato bali  zingejikita katika kubuni na kuibua miradi ya maendeleo  ili kujikwamua kiuchumi na kujiongezea vitega uchumi vitakavyoleta maendeleo katika Halmashauri zao

“ Kusipokuwa na ubunifu, kujitoa  katika utendajikazi wa watumishi wa Halmashauri, hali ya unyafuzi wa mapato itaendelea na  bado Halmashauri nyingi zitakuwa ni tegemezi kwa Serikali, hivyo  ninaziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanabuni vitega uchumi  ili waweze kujitegemea kwa kutumia mapato yao ya ndani ” Anasisitiza Mhe.Jafo

Mhe. Jafo amezitaka Halmashauri zote nchini kuiga mfano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kubuni  Miradi ya Maendeleo  kwa ajili ya  vitega uchumi  na kuondokana na utegemzi kwa Serikali.

Amefafanua zaidi kuwa watumishi wa Serikali za Mitaa nchini kuacha kufanyakazi kwa maigizo, kwa kujionyesha kwenye mitandao  bali wafanyekazi kwa weledi  lengo likiwa ni kuwahudumia wananchi maskini na kulipeleka taifa katika uchumi wa kati

“Kuna watu nchi hii wamezoea maigizo, hivyo kwa wale ambao wapo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuacha kufanyakazi kwa maigizo bali watu wafanyekazi kwa weledi ili kufikia mallengo ya Serikali.” Amesisitiza Mhe. Jafo

Amesema watu wasipende kujionyesha kwenye mitandao kuwa wanafanyakazi , bali wafanye kazi kwa ajili kulitumikia taifa hasa wananchi maskini  kwa kuwa nchi hii inabadilika na kinachohitajika ni maendeleo ya Taifa.

Amewasii vijana waliopewa dhamana ya uongozi nchini kufanyakazi kwa bidii na maarifa waliyonayo na kuacha kufanyakazi kwa maigizo, lengo likiwa ni kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika kufikia uchumi wa kati.

Amewapongeza  Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuweza kutumia Makusanyo ya Fedha za Ndani kwa ajili ya ujenzi wa vitega uchumi lengo kubwa ni kutoa unyafunzi wa mapato na  kupunguza utegemezi kwa Serikali.

 Wakati huohuo Mkurugenzi wa Halmashauri wa Jiji la Dodoma Bw.  Godwin Kunambi amesema ujenzi wa jengo la Hoteli “Dodoma City Hotel” litajengwa katika eneo la Paradise barabara ya Nyerere kwa gharama ya shilingi bilioni 9.9 kutoka katika nyanzo vya mapato ya ndani  lengo likiwa ni kupunguza utegemezi kwa Serikali, kuongeza ajira kwa wananchi wa Dodoma, kutoa huduma bora kwa wananchi, kuboresha mji wa Dodoma na kupunguza umaskini na kuongeza kipato kwa wananchi wa Dodoma

Bw. Kunambi ameendelea kusema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inategemea kujenga kitega uchumi Mji wa Serikali “Government City Complex “kwa gharama ya shilingi bilioni 59.3 ambapo kutakuwa na ofisi, maduka,Kumbi za Mikutano, Maegesho ya Magari, Maeneo ya mabenki, migahawa bna maeneo ya mahoteli.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge amesema kuwa kupitia miradi hiyo  Wananchi wa Mkoa wa Dodoma watapata fursa ambazo zitawasaidia kuongeza kipato  na kukuza uchumi wa Dodoma utaongezeka.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.