• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Jafo Aagiza Halmashauri Kutenga Fedha Kukarabati Samani za Shule

Imewekwa tar.: February 21st, 2020

Serikali imeziagiza halmashauri zote nchini kukarabati samani za shule kupitia fedha zinazopelekwa shuleni za program ya Elimu Bila Malipo ili kuondoa tatizo la madawati kwenye shule nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo wakati akipokea taarifa ya tafiti iliyofanya kati ya Chuo Kikuu cha Dodoma na taasisi ya Mdigri Logistics kuhusu vifaa vya Ufundishaji na Ujifunzaji kwenye shule za sekondari iliyofanyika katika mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Jijini Dodoma.

“nielekeze Mamlaka za Serikali za Mitaa katika halmashauri zote kupitia Wakurugenzi, kupitia na kushughulikia madawati na meza zote zinakarabatiwa kupitia fedha za Elimu Bila Malipo”

Jafo amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia vikundi vya vijana kufanya ukarabati wa miundombinu ya madarasa, madawati na vifaa vingine vya shule ikiwa ni sehemu ya kuwapa ajira vijana na kuboresha mazingira ya elimu katika shule zilizopo kwenye mamlaka zao badala ya kusubiri kutenga fedha kutengeneza madawati mapya.

“halmashauri zitumie vikundi vya vijana kufanya uakarabati wa miundombinu ya madarasa, madawati na vifaa vilivyopo katika shule, haiwezekani kusubiri kutenga fedha za  madawati mapya wakati yapo madawati ya zamani na hayajakarabatiwa” alisema Waziri Jafo.

Waziri Jafo amesema pamoja na watendaji hao kukarabati samani za shule pia wakarabati miundombinu ya shule yakiwemo majengo, matundu ya vyoo, madarasa na miundombinu mingine kwenye sekta ya elimu yaweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.

Aidha amewataka Wakuu wa shule kuendelea kusimamia masuala ya kitaaluma, mazingira na miundombinu kama kipaumbele chao na kuboresha hali ya taaluma nchini.

Jafo amewataka watafiti hao na wengine kuendelea kufanya tafiti kwenye sekta ya elimu na kuyapa kipaumbele maeneo mengine kama miundombinu ya vyoo, madarasa na vinakilishi ili kutoa mchango wa kufanya maboresho kwenye elimumsingi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Benilith Saatano Mahenge amesema watafiti wamefanya tafiti na kubaini tunalo tatizo katika eneo la elimu na kwamba watanzania hatuna utamaduni wa kukarabati madawati na miundombinu hivyo tafiti itatusaidia kuboresha miundombinu kwenye sekta ya elimu.

Awali Dkt. Ombeni Msuya kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma aliwasilisha taarifa ya tafiti ya vifaa vya Ufundishaji na Ujifunzaji kwenye shule za sekondari 35 na kusema kuwa utafiti huo umefanyika kwenye halmashauri 7 zote za mkoa wa Dodoma kuanzia mwezi Januari, 2019 hadi januari, 2020 na kubaini changamoto kadhaa yakiwemo kutokuwepo kwa zana za kufundishia zinazokidhi mahitaji, kuwepo kwa viti, meza na vifaa vya maabara visivyo na ubora, kuwepo kwa meza 91,000 na viti 915 ambavyo havitumiki na vinahitaji ukarabati mdogo.

Dkt. Msuya ametoa rai kwa Serikali kuundwa kwa kikundi kazi kitakachokuwa kinakarabati samani na miundombinu ya shule ‘Maintainance Mobile Unit’ ambao wanaweza kutoka katika vyuo vya ufundi ili kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia shuleni.

Kwa upande wake Yoram Mkwawa Mkuu wa shule Mbabala ametoa rai ya kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu Sera ya Elimu Bila Malipo kwani kuna upotoshwaji mkubwa kuhusu sera hiyo ambapo wazazi hawapo tayari kuchangia chochote kwa ajili ya maendeleo ya shule zao lakini pia amewataka Wakuu wa shule kuwa wabunifu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali shuleni badala ya kusubiri fedha kutoka Serikalini.

                   Anaandika Fred Kibano

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.