• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

JAFO AWATAKA TEMEKE KUKAMILISHA MIRADI YA DMDP KWA UBORA

Imewekwa tar.: July 20th, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Dar es Salaam na leo ametembelea  Manispaa ya Temeka kukagua maendeleo ya mradi wa uboreshaji wa miundombinu unaotekelezwa kupitia mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (DMDP).

Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Jafo ametembelea na kukagua ujenzi wa masoko ya kisasa yanayojengwa katika Kata ya Kijichi na  Mbagala Kuu, Kituo cha Mabasi madogo sambamba na  Ujenzi wa barabara za mitaa inazojengwa kwa kiwango cha Lami katika Kata hizo.

Akitembelea maeneo ya miradi Mhe. Jafo alisisitiza ubora wa miradi hiyo pindi itakapokamilika na kuwataka Wakandarasi wajenzi kukahikisha wanaongeza umakini na kuzingatia ubora katika kila hatua ya ujenzi huku wakijali muda uliowekwa wa ukamilishaji wa miradi hiyo.

“Fedha za miradi hii  zipo zinasubiria kazi tu ikamilike lakini sio kukamilika chini ya kiwango. Kinachotakiwa na nyie wakandarasi mnazingatia Mikataba mliongia mwanzoni kabla hamjaanza kazi na kufikia viwango vile vilivyowekwa ili Fedha itakayolipwa iendane na kazi iliyofanyika” alisema Mhe. Jafo.

Akiwa katika Soko la Kijichi Mhe, Jafo amesema ameridhishwa na ujenzi unaondelea ila pia amewataka uongozi wa Temeke pamoja na Mkandarasi kutoa ajira ndogondogo kwa vijana wa maeneo hayo ili nao waweze kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Temeke Mhe. Issa Mangungu amesema hatasubiria tena Mhe. Waziri Jafo aje kukagua miradi hii ndio na yeye afike kwenye maeneo hayo bali ataweka ratiba katika kila wiki kuhakikisha anapitia miradi yote kuona maendeleo ya ujenzi na kuhakiki ubora wa miundombinu hiyo itakayoongeza thamani ya Manispaa ya Temeke kwa ujumla.

Akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Miradi Mratibu wa Dmdp Manispaa ya Temeke Edward Haule amesema  kwa sasa wameanza kutekeleza  mradi huu katika Kata 8  kati ya 23 zinazohusika na katika maeneo yote hayo wanaboresha miundombinu msingi  ambayo ni kichocheo cha ustawi wa jamii husika.

Katika Kata ambazo zimetembelewa leo na Mhe. Waziri Jafo hususan ni Kata ya Kijichi kazi zinazoendelea ni ujenzi wa barabara 13 zenye urefu wa Km 18.7, Soko moja lenye uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 200, kituo kimoja cha daladala, mfumo wa maji utakaohudumia wakazi zaidi ya 300,000 na taa za barabarani 700  kwa gharama ya Tsh Bil. 22.

Aliongeza kuwa katika Kata ya Mbagala Kuu kazi zitakazofanyika ni ujenzi wa barabara 12 zenye urefu wa Km 12, soko moja lenye uwezo wa kubeba wafanyabiashara  zaidi ya 290, kituo cha daladala, mfumo wa maji utakaohudumia wakazi zaidi ya 400,000 na Taa za barabarani 600 kwa gharama ya Tsh Bil. 19.

Miradi hii itakayoleta manufaa makubwa kwa Manispaa ya Temeke na kwa wananchi kwa ujumla  inategemewa kukamilika mapema mwezi Januari mwaka 2019.


Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.


Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.