• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Jafo atoa Neno kwa Plan International

Imewekwa tar.: May 23rd, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(Mb) amelitaka Shirika la Plan International kutekeleza miradi yake hapa nchini kwa weledi na umakini ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kupata ufadhili.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kufunga warsha ya Shirika hilo iliyokuwa na lengo la kufanya tathimini na kuweka mipango ya Shirika iliyofanyika Jijini Dodoma.

Alisema kuwa ni vyema Shirika la Plan International kutekeleza majukumu na miradi yake kwa ufanisi mkubwa ili kushika nafasi ya kwanza kwa utendaji kazi kwa Nchi zinazotekeleza miradi yake mashariki na kusini mwa Africa (RESA).

“Ninyi wataalamu wa Shirikia la Plan International mnatakiwa kuchapa kazi kwa weledi wa hali juu ili kushika nafasi ya kwanza na kuwa katika nafasi nzuri ya kupata ufadhili wa utekelezaji wa malengo ya Shirika.”

Jafo aliongeza: “Ujue ufadhili ndio kila kitu katika Shirika, mkifanya kazi vizuri mtapata fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na hapo mtaweza kuwafikia wanufaika wengi katika achi yetu na kuzidi kuwainua na kuleta matumaini mapya katika jamii yetu,” Alisema Jafo.

“mkizidi kupata ufadhili ndipo na nyie mtapata mishahara mizuri na marupurupu hivyo ufadhili sio kwa sababu ya wananchi pekee bali ni kwa faida yenu  kama watendaji wakuu wa shirika hili”

Aidha, Jafo alitumia fursa hiyo kuwapongeza Plan International kwa namna wanavyofanya kazi zao jambo ambalo linachangia utoaji wa huduma bora kwa jamii.

“Mimi nimefanya kazi Plan International na umahiri wangu na weledi katika utendaji kazi umetokana na kufanya kazi katika Shirika hili limenijenga katika misingi ambayo mpaka kazi imekuwa ni sehemu ya masiha yangu na wala sichoki kufanya kazi hii ndio Plan International”Alisema Jafo.

“Watu wengi wamekuwa wakinishangaa kwa kazi nyingi ninazozifanya kwa siku na bado nazifanya kwa umakini na umahiri mkuwa msingi huu niliupata Plan Internatioinal na bado  nawaelekeza watumishi wa Wizara yangu kufanya kazi kwa bidii wakati wote ndio maana unaona mabadiliko makubwa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Naye Meneja Ufadhili wa Plan International Nicodemus Gachu alisema kuwa mpaka sasa Shirika lina watoto rafiki elfu 30 ambao wanapata huduma mbalimbali kutoka Plan International.

Gachu alisema kwa sasa Plan Internationa imekuja na mpango wa kutoa Bima ya Afya iliyoboreshwa kwa watoto rafiki wa shirika hilo, ambao unatarajia kuzinduliwa hivi karibuni kwa kuwakabidhi watoto hao Bima za Afya katika kila Mkoa ambako wana watoto rafiki.

Gachu alitumia fursa hiyo kuanisha kazi ambazo Shirika limezifanya kuwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya Afya katika baadhi ya hospital na vituo vya Afya kama Buguruni, ujenzi wa miundombinu ya Elimu, ujenzi wa  miundombinu ya Maji, kuwawezesha vijana kiuchumi na kuwajengea uwezo watoto kuzifahamu hazi zao.

Naye Neema Moris ambaye ni Meneja ya Uniti ya Kisarawe amesema kupitia warsha hiyo ya siku nne wameweza kujitathmini utendaji kazi wa shirika, namna ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika maeneo ya kazi na kuweka malengo ya utekelezaji wa kazi za Shirika.

Ikumbukwe kuwa Waziri Jafo alianzia kazi katika Shirika la Plan Internationa akiwa kama Meneja wa Uniti ya Kisarawe kabla ya kuwa Mbunge wa Kisarawe kisha kuteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Mwisho.

Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.