• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Jafo ataka ifikapo Oktoba 30, Mikoa yote ikamilishe mchakato wa zabuni za watoa dawa

Imewekwa tar.: October 9th, 2018

Na Mathew Kwembe,Dar es salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote 26 nchini kuhakikisha kuwa ifikapo tarehe 30 oktoba, 2018 mikoa ambayo haijakamilisha zoezi la kuwapata wazabuni teule wa kutoa huduma ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika hospitali za wilaya na vituo vya afya katika mikoa yao wawe wamekamilisha zoezi hilo ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi hasa pale huduma hizo zinapokosekana katika Bohari kuu ya Dawa ya Taifa (MSD).

Aidha, Waziri Jafo alisema kuwa mara baada ya tarehe 30 Oktoba 2018, hataki kusikia kuwa kuna kituo cha afya ambacho hakina dawa au vifaa tiba.

Akizungumza jana wakati wa hafla fupi ya uanzishaji na utekelezaji wa Mfumo wa Jazia ambao unalenga kuviwezesha vituo vya kutolea huduma za afya kupata mahitaji yake ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi pale huduma hizo zinapokosekana kutolewa na Bohari kuu ya Dawa ya Taifa, Waziri Jafo alisema kuwa baada ya tarehe hiyo vituo vyote vihakikishe  kuwa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vyao usipungue asilimia 98.

“Baada ya tarehe 30 Oktoba, nawaagiza wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa wanasimamia mikoa yao katika zoezi hili la upatikanaji wa dawa. Sitaki kusikia kituo cha afya hakina dawa,” alisema Waziri Jafo.

Alisema mtu anapokwenda kwenye zahanati au kituo cha afya kwa ajili ya kupata huduma ya matibabu anategemea huduma hizo azipate kwenye vituo hivyo na si vinginevyo, hivyo ni jukumu la vituo hivyo kuhakikisha vinakuwa na dawa za kutosha ili kuwahudumia wananchi kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya chama cha Mapinduzi.

Alifafanua kuwa mfumo huo ujulikanao kama mfumo jazia  ulikubalika kuanza rasmi na serikali kwa nchi nzima na kutamkwa katika ukurasa wa 36 wa Ilani ya uchaguzi  Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ambayo ilielekeza kuwepo na Health Sector strategic plan,  na pia azimio la kikao cha waganga wakuu wa mikoa na wilaya cha mwaka 2017.

Waziri Jafo alielekeza kuwa sambamba na juhudi hizo za kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana za kutosha kwenye vituo vya afya na zahanati, pia alirudia agizo lake alilolitoa awali la kuwepo na udhibiti wa kutosha wa mifumo ya fedha kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

“Pamoja na control (udhibiti) ya upatikanaji wa dawa, tuhakikishe kuwa vituo vya kutolea huduma za afya vinatumia mifumo ya fedha iliyowekwa ili kudhibiti upotevu holela wa fedha za umma,” alisema na kuongeza:

“Niliagiza watu watumie mifumo ya fedha lakini tumebaini kuwa zaidi ya robo tatu ya fedha zinakusanywa nje ya mfumo wa fedha (Gothomis).”

Aidha Waziri Jafo alisema kuwa serikali imetumia fedha nyingi katika kuhakikisha kuwa inaboresha hospitali na vituo vya afya nchini.

Aliongeza kuwa tangu nchi ipate uhuru hadi mwaka 2015 kulikuwa na vituo vya kutolea huduma za afya vipatavyo 515 ambavyo kati ya hivyo 115 ndivyo vilivyokuwa vikitoa huduma ya upasuaji lakini katika kipindi cha miezi 12 iliyopita jumla ya vituo vya kutolea huduma ya afya 210 vilijengwa nchini.

Sambamba na hilo, katika kipindi cha miezi 18 ijayo serikali inatarajia kukamilisha ujenzi wa vituo vingine 343 ambavyo pia vitaweza kutoa huduma ya upasuaji.

Pia Waziri Jafo alisema kuwa nchi yetu tangu uhuru kulikuwa na hospitali za wilaya 77 tu, lakini mwaka huu serikali inatarajia kukamilisha ujenzi wa hospitali za wilaya 67 nchi nzima ambapo kati ya hizo Mkoa wa Dar es salaam zitajengwa hospitali mpya tatu katika wilaya za Ilala, Kigamboni na Ubungo.

“Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli ametoa kiasi cha shilingi bilioni 33.5 kwa ajili ya kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha wa 2018/2019,” alisema Waziri Jafo

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Zainab Chaula aliusifu kutanuka kwa mfumo wa jazia kwani katika zoezi la majaribio katika mikoa ya Dodoma, Shinyanga na Morogoro ulionyesha mafanikio makubwa.

Alisema kuwa mfumo huu ambao upatikanaji wa bidhaa za afya hutumia fedha za mapato na makusanyo ya kituo cha kutolea huduma za afya na siyo ruzuku ya serikali.

Dkt Chaula alisisitiza kuwa mfumo huo utakwenda kusaidia pale Bohari kuu ya Dawa itakuwa imefikia na pindi Bohari kuu ya dawa inapotoa asilimia 100 mfumo huu  hautafanya kazi.

Aliongeza kuwa kutokana na ukubwa wa nchi, upo uwezekano wa Bohari Kuu ya Dawa kushindwa kuyafikia baadhi ya maeneo ndiyo maana serikali imekuja na mfumo wa jazia ili kuondoa kero iliyokuwa ikivipata baadhi ya vituo vya kutolea huduma ya afya hasa vile vilivyopo pembezoni mwa nchi.




Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.