• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Jafo alaaani vitendo vya watumishi kutumia nguvu dhidi ya wananchi

Imewekwa tar.: February 6th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amelaani vikali vitendo cha watumishi wa umma kutumia nguvu nyingi dhidi ya wananchi hali inayopelekea kuletea machafu kwenye jamii na hata kupelekea mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia.

Jafo amelaani vitendo hivyo wakati wa mazishi ya marehemu Isaka Petro aliyefariki  jumamosi katika vurugu zilizotokea katika kanisa la Waadiventisti Wasabato Itigi kundi Namba Two na kuzikwa nyumbani kwao kijiji cha kazikazi kata ya Kitaraka;  Mazishi hayo pia yamehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Singida pamoja na Wilaya ya Manyoni.

Jafo amesema tukio hilo lilitokea sio agizo la Serikali na waliotekeleza wamefanya kwa utashi na akili zao binafsi na hawakuagizwa na mtu yeyote na zaidi wametenda kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.

“Hakuna namna tunaweza kusema vinginenevyo kuhusu tukio hili zaidi ya kuwa tukio baya na la kusikitisha sana kuwahi kutokea kwa wananchi wetu, tena likiwa limetekelezwa na watumishi wa Serikali inasikitisha sana nawasihi watumishi wa umma tutangulize utu mbele katika kila kazi tunazozifanya”

Aliongeza kuwa watumishi wa umma haijalishi unafanya kazi gani katika mazingira gani lakini hakikisha unatanguliza ubinadamu kwanza ili tulinde maisha yetu na ya wale tunaowahudumia haipendezi wewe ukawa chanzo cha mtafaruku katika jamii tusaidie kuwaunganisha wananchi na kuwafanya kuwa kitu kimoja na sio kuwa chanzo cha ugomvi na mafarakano.

Kwa taarifa nilizopewa na nimezithibitisha ni kuwa wote waliohusika na tukio hili wameshakamatwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama bado vinaendelea na taratibu zao alisema Jafo.

Katika msiba huo Waziri Jafo akiwa na viongozi wa Mkoa wa Singida alitoa pole kwa familia ya marehemu sambamba  na rambirambi pia alishirikiana na  ndugu, jamaa na marafiki katika shughuli zote za mazishi ya marehemu Isaka Petro nyumbani kwao kazikazi.

Akizungumza katika mazishi hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi  amesema kuwa msimba huo ni pigo kwa Serikali pamoja na wananchi wote wa kijiji cha kazikazi.

“Serikali inawahudumia wananchi walio hai na sio wafu sasa mwananchi wetu anapotutoka tena kwa kifo cha kwa namna hii na sisi tunapata pigo kwa sababu dhamira yetu ya kufikisha huduma bora kwake haitafikiwa”

Sisi kama Serikali tuna wajibu wa kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya wananchi wetu kufanya shughuli zao kwa usalama wa hali ya juu sasa wajibu huu unapotekelezwa kinyume na taratibu zetu ni makosa ninatoa na kila mtu atawajibika kwa kadiri ya kosa lake alisema Dkt. Nchimbi.

Aidha Dr Nchimbi aliwaeleza wananchi wa kazikazi pamoja na Kitaraka kuwa wale wote wanaolima katika Shamba la Kitaraka waendelee na shughuli zao kama kawaida na wasilipe ushuru wa shilingi elfu ishirini kama ilivyokuwa hapo awali mpaka hapo yatakapokuja maelekezo mengine.

“Watumishi wa halmashauri mupeleke ujuzi na pembejeo kwa wakulima wadogo wa shamba la Kitaraka na sio kwenda kuwabugudhi kwa kuwadai ushuru nyie endeleeni na wawekezaji wenu wakubwa kwa kadiri ya makubalino mliyoingia lakini hawa wananchi  wanaolima ekari moja moja waacheni waendelee na kilimo chao” alisema Dkt. Nchimbi.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato Itigi Kundi Namba Two Manigina F.S Manigina aliwaasa wanakijiji cha kazikazi kutokua na kisasi na kumuomba Mungu ili tukio kama hilo lisitokee tena katika kijiji chao.

“Visasi ni vya Mungu nyinyi msiweke visasi na mtu ila endeleeni na maisha yenu kama kawaida na Mungu atazidi kuwashushia baraka zake katika kazi zenu” alisema Mchungaji Manigina.

Katika vurugu zilizotokea siku ya jumamosi katika kijiji cha kazikazi eneo la Kanisa la Waadiventista Wasabato Kundi Namba Two baina ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi akiwa na askari wa wanyamapori na baadhi wa wananchi wa kijiji hicho zilipelekea kifo cha kijana Isaka Petro mwenye umri wa miaka 28.

Marehemu ameacha mke na watoto watatu.

Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Mweli awatega Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu kwenye Mfumo wa PREM/PREMS.

    January 10, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.