• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Book History
    • Kuhusu Wizara
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Utawala
    • Directory
    • Vitengo
    • Muundo wa Wizara
    • Mikoa, Wilaya na Halmashauri
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji

Jafo akagua tena ujenzi wa Hospitali ya Uhuru

Imewekwa tar.: July 15th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Selemani Jafo amefurahishwa na hatua za awali za ujenzi wa hospital ya Uhuru inayojengwa katika eneo la Chamwino Mkoani Dodoma kwa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk John Magufuli.

Mhe.Jafo amesema  amefanya ziara  maalumu ya kukagua ujenzi wa Hospitali hii ya Uhuru baada ya kufika katika eneo hilo  mnamo mwezi Juni  na kukuta hakuna chochote kilichoanza kufanyika na hata eneo lilikuwa halijasafishwa hali ile ilinifedhehesha sana.

”Nilikuja hapa  Juni 19 kukagua  eneo hili  sikuridhishwa baada ya kukuta ujenzi haujaanza ndio maana nikatoa maelekezo kwamba ujenzi uanze mara moja kwa kutumia kikosi maalumu cha Jeshi ili kutimiza azma ya Mhe. Rais katika kutoa huduma bora za Afya karibu na wananchi, leo naona  tayari wenzetu wa Suma JKT wameshaanza kazi hili limenifurahisha,” amesema Mhe Jafo.

Hivi ndio tunavyotakiwa tufanye kazi sio mnapewa maelekezo alafu mnaanza kujivuta vuta kufanya vikao visivyoisha hiyo haipendezi kwa sababu mnawacheleweshea Wananchi huduma aliongeza Jafo.

Nimefurahi zaidi kuona  eneo lote la Ekari 40 limeshasafishwa ikiwemo kujenga uzio pamoja na ofisi za wafanyakazi wajenzi pia vifaa vimeshaanza kufikishwa katika eneo hili la hospitali na TBA wako wanaendelea na kazi yao ya usimamizi na ushauri hongereni kwa hilo alisema Jafo.

”Kwa kweli leo nimeridhishwa na hatua ya awali ambayo tumefikia katika ujenzi wa Hospitali hii, na niwaombe wataalamu wangu kuacha kufanya kazi kwa mazoea na tunapotoa maagizo basi wayatekeleze kwa wakati, ni matarijio yetu hadi kufikia Januari, 2020 tutakua tumeshakamilisha ujenzi huu,” amesema Mhe Jafo.

Kwa upande wake Mhandisi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania TBA, Mhandisi Daniel Mwakasungura amesema Hospital hiyo ya Uhuru itakuwa ni ya gorofa moja na itatumika ramani ya Hospital ya Tunduma iliyoboreshwa.

“Ramani iliyopendekezwa ambayo ni Hospital ya Tunduma tunaendelea kuiboresha kulingana na mahitaji na viwango vya Hospital ya Uhuru na sisi kama TBA tutasimamia suala la hili la ramani na kutoa ushauri wa mradi huu mpaka pale utakapokamilika” Alisema Mwakasungura.

Akizungumzia bajeti ya mradi mzima Mwakasungura amesema fedha  iliyotengwa ambayo tumeingia mkataba na Suma JKT ni Shilingi Bilioni 3 ambazo zitajenga majengo yote yanayohitajika  na tunatarajia mradi huu utakamilika  baada ya miezi sita kama ambavyo tulievyoelekezwa,” amesema Mwakasungura.

Nae Mhandisi wa Suma JKT, Luteni Kanali Onesmo Njau amesema walikabidhiwa jukumu la ujenzi huo Juni 19 mwaka huu na tayari washatekeleza maelekezo kutoka kwa Mhe Jafo ikiwemo kuandaa ofisi, sehemu za kuishi kwa watendaji na muda sio mrefu wataanza ujenzi ili kukamilisha mapema kama ilivyoelekezwa.

Hospitali hiyo inajengwa baada ya Rais Magufuli kuelekeza kufanya hivyo katika sherehe za Uhuru mwaka 2018 ambapo alifuta sherehe hizo na kupeleka Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hizo kujenga Hospitali ya Uhuru mkoani Dodoma.


Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 TANZANIA BARA December 06, 2019
  • TANGAZO LA KUWAREJESHA WAGOMBEA WASIO NA MAKOSA YA KIKANUNI KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019 November 10, 2019
  • MAELEZO KUHUSU ZOEZI LA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU ZA MAOMBI YA UTEUZI WA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI October 30, 2019
  • TANGAZO NA ORODHA YA WALIOITWA AJIRA ZA MKATABA TAASISI YA BENJAMIN MKAPA October 25, 2019
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA YA AFYA REPLACEMENT October 25, 2019
  • Orodha ya Majina ya watumishi wa Ajira Mpya kada ya Afya September 18, 2019
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Jafo atangaza waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza, 2020

    December 05, 2019
  • Jafo ambana Mkandarasi SKOIL Building Contractors Limited

    December 04, 2019
  • Jafo akagua ujenzi wa hospitali ya Uhuru

    December 04, 2019
  • Halmashauri zapigwa marufuku kukopa Benki

    November 29, 2019
  • Angalia zote

Video

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Dodoma
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.