• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Kitabu
    • Kuhusu Wizara
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mikataba wa Huduma kwa mteja
  • Utawala
    • Idara
    • Vitengo
    • Muundo wa Wizara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Mpango Miji Mkakati (TSCP)
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi
    • Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Machapisho
    • Hotuba ya waziri
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti
    • Majarida
    • Vipeperushi
    • Fliers
    • Burners
    • Sticker
    • Fomu Mbali mbali
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
  • Simulizi za Wizara yetu
    • Wazo la Waziri

Hati Safi zimeongezeka katika Mamalaka za Serikali za Mitaa

Imewekwa tar.: April 13th, 2018
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amesema katika Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Halmashauri zilizopata Hati Safi zimeongezeka  kutoka Halmashauri 81 kwa mwaka 2015/16 mpaka kufikia Halmashauri 166 (90%) kwa mwaka  2016/17.

Jafo ameyasema hayo wakati kwa Kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ukumbi Bunge kuhusu utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo ya CAG kwa hesabu za Mamlaka za Serikali  za Mitaa kwa  mwaka Ulioishia  Juni 30, 2017.

Alisema “napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa maelekezo yao mazuri yaliyosaidia sana utendaji kazi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na MSM; Michango yao, ushauri na maelekezo yamewezesha kuongeza Idadi ya Hati Safi.

Akizungumzia kuhusu hoja zilizobainishwa katika ropoti ya CAG Mhe. Jafo alisema tumefanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa katika ripoti zilizopita ambapo watumishi 434 wamechukuliwa hatua baada ya kubainika kusababishia halmashauri zao hasara/hoja zisizo za lazima kutokana na kutotekeleza ipasavyo wajibu wao ama kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu.

“Kati ya hao 9 wamefukuzwa kazi, Watumishi 210 wamepewa barua za onyo huku Watumishi 15 wakifikishwa kwenye vyombo vya dola. Watumishi 28 wamesimamishwa kazi, 13 wametakiwa kufidia hasara kutoka kwenye mishahara yao wengine 4 wameshushwa vyeo na wengine 10 wamebadilishiwa majukumu” alisema Jafo.

Aliongeza kuhusu MSM kupokea Fedha pungufu ya Bajeti Iliyoidhinishwa ni kwa sababu Serikali hutegemea makusanyo ya mapato kutoka vyanzo mbalimbali. Hivyo, kiasi kinachotumwa kwenye MSM hutegemea mwenendo wa mapato yaliyopatikana lakini pia fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa na Serikali kwa mwaka wa fedha uliotaguliwa 2016/17 zimeongezeka ikilinganishwa na mwaka  wa 2015/16.

Kwa  mwaka 2016/17 fedha za miradi ya maendeleo zilizopokelewa na MSM ni Tsh. 705,927,921,596.20 sawa na 57% ya bajeti iliyoidhinishwa ya Tsh. 1,242,616,839,000 akati mwaka 2015/16, fedha zilizopokelewa  zilikuwa ni Tsh. 390,525,992,297 sawa  39%  ya bajeti ya Tsh. 1,010,650,744,099.

Kuhusu changamoto katika Usimamizi wa Mapato katika Mhe. Jafo alieleza Wizara imeendelea kuziba mianya ya uvujaji wa mapato kwa kuhakikisha kuwa Halmashauri zinahamia katika matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato ujulikanao kama Local Government Revenue Collection and Information System (LGRCIS) ambapo takwimu zote za mapato zinatunzwa katika mfumo huo ambao pia umeunganishwa na mashine za kukusanyia mapato (Point of Sales) zinazotumiwa na Mawakala/Wakusanya mapato, na hivyo kuiwezesha Halmashauri kufahamu mapato  yaliyokusanywa na Wakala/Wakusanya mapato hao.

Vile vile, mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya benki, na hivyo kuwezesha Halmashauri kufahamu kiasi ambacho Wakala/Mkusanya mapato amekiingiza kwenye akaunti ya benki ya Halmashauri ikilinganishwa na kiasi alichokusanya. Mpaka sasa, Halmashauri zote 185 tayari zimewekewa mfumo huu wa LGRCIS.

Wakati huo huo alieleza Kuhusu Vitabu 379 vya Kukusanyia Mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa Wakaguzi amesema  Licha ya kuwa  idadi ya Halmashauri na idadi ya vitabu vya kukusanyia mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa Wakaguzi imepungua kutoka  871 katika Halmashauri 57 kwa mwaka 2015/16 mpaka vitabu 379 katika Halmashauri 21 kwa Mwaka 2016/17, OR – TAMISEMI imeendelea kusimamia maelekezo ya Serikali ya Halmashauri zote ziachane na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia stakabadhi/vitabu vya kuandikwa kwa mkono, na badala yake mapato yakusanywe kwa kutumia mashine za kielektroniki.

Waziri Jafo alimalizia kwa kutolea ufafanuzi wa Soko la Mwanjelwa –Mbeya na kusema kuwa OR-TAMISEMI imeanza kuchukua hatua kuhusiana na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa na kwa kuanza tulimuomba CAG kufanya ukaguzi maalum na taarifa iliashiria makosa ya kijinai na tayari Serikali imelifikisha suala hili kwenye vyombo vya Dola, ambapo pia Wahusika Wakuu wa mikataba husika na usimamizi wa utekelezaji wake, nao pia wameshafikishwa kwenye vyombo vya Dola kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi. Serikali itaendelea kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na CAG ili kuokoa hasara itokanayo na ujenzi wa soko hilo.


Matangazo

  • Michoro ya Majengo ya Afya February 10, 2018
  • Waliondolewa kwenye "Payroll" Kurejeshwa March 07, 2018
  • Tangazo la Marekebisho ya vituo vya kazi kwa Watumishi kada ya Afya February 16, 2018
  • Uhamisho wa Watumishi March 26, 2018
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Jafo apiga marufuku uchimbaji wa mchanga kwenye mito ya Dar es salaam

    April 20, 2018
  • Wadau wa dawa watakiwa kuchangamkia fursa

    April 18, 2018
  • Astashahada, Stashahada Msizipe Kisogo: Waziri Jafo

    April 18, 2018
  • Bajeti TAMISEMI Yapita kwakishindo

    April 17, 2018
  • Angalia zote

Video

Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Maji
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Maliasili na Utalii
  • Wizara ya Elimu
  • Wizara ya Nishati na Madini
  • Wizara ya Kilimo
  • Wizara ya Mambo ya ndani

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

click here

    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sera ya faragha
    • Onyo
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.