• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Halmashauri zavunja rekodi, ukusanyajiwa mapato ya ndani

Imewekwa tar.: August 14th, 2019

Kwa mara ya kwanza Nchini Halmashauri zote 185 zimefanikiwa kukusanya sh. bilioni 661.4 ambayo ni sawa na asilimia 91 ya malengo ya mwaka wa Fedha 2018/19 ya kukusanya sh bilioni 723.

Matokeo haya ni ongezeko la asilimia 9 kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 ukilinganisha na makusanyo ya asilimia 81 ya Mwaka wa Fedha 2017/18 huku Halmashauri ya Jiji la Dodoma sambamba na Mkoa wa Dar es salaam zikiongoza kwa mapato ghafi.

Hayo yabamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa alipokuwa akitoa  taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za vyanzo vya ndani vya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/19. Mapato haya ya ndani hayijumuishi vyanzo vinavyokusanywa na Serikali kuu.

Akifafanua zaidi Mhe. Jafo alisema halmashauri za Wilaya tano zilizoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi(asilimia 171),  Wanging’ombe(asilimia 165), Kilolo (asilimia 150), Misenyi (asilimia 142) huku Mbeya Dc ikishika nafasi ya tano kwa kukusanya asilimia 141.

Halmashauri  za Wilaya zilizofanya vibaya kiasilimia ni Tandahimba Dc (asilimia 19), Msalala (asilimia 19), Masasi Dc (asilimia 26) Newala (asilimia 27) pamoja na Nanyumbu (asilimia 36).

Kwa kigezo cha pato ghafi, Mhe. Jafo alisema halmashauri zilizoongoza kwa wingi wa mapato kuwa ni Halmashauri ya Jiji la Dodoma (Sh bilioni  71.7), Ilala (Sh bilioni 58.1), Kinondoni(Sh bilioni 34) Temeke  Sh bilioni 33.3), Ubungo Mc (bilioni 18.6) na Jiji la Arusha (Sh bilioni 16.4) wakati halmashauri tano zilizofanya vibaya katika kundi hili ni Nanyamba (sh milioni 258), Gairo Dc(Sh milioni 396), Kigoma Dc (Sh milioni 397.1) Buhigwe (Sh milioni 403.8) na Kakonko Dc (Sh milioni 403.8).

Aidha, katika kundi la mikoa kwa kigezo cha asilimia, Jafo alisema mikoa inayoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani ni Mkoa wa Geita (asilimia 119), Iringa (asilimia  117),Songwe (asilimia 112), Kagera (asilimia 105) na Njombe  (asilimia  104), wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Mtwara (asilimia 42), Simiyu (asilimia  459), Shinyinga (asilimia 62), Kigoma (asilimia 74) Mara na Morogoro (asilimia 80).

Kwa upande wa mikoa kwa kigezo cha pato ghafi, Mhe. Jafo alitaja Mikoa inayoongoza kuwa ni Dar es Salaam (Sh bilioni1 163.5) Dodoma (Sh bilioni 82.6), Mwanza (Sh bilioni 32.6) Arusha (Sh bilioni 31.9) na Mbeya (Sh bilioni 31.4) wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Katavi (Sh bilioni 7.3), Kigoma (Sh bilioni 7.7), Rukwa (Sh bilioni 8.2) Simiyu (Sh bilioni 8.8) na Njombe (Sh bilioni 11.4).

Aidha, Jafo alisema Jiji la Arusha  limeongoza  katika kundi la halmashauri za majiji kwa asilimia kwa kukusanya asilimia 105 ya makisio huku jiji la Mbeya  likiwa la mwisho katikakundi hilo baada ya kukusanya asilimia 89 ya makisio.

Alisema Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaongeza kwa kigezo cha pato ghafi ambapo imekusanya Sh bilioni 71.7 na halmashauri ya jiji la Mbeya imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya Sh bilioni 11.4.

Aidha, Jafo alisema halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imeongoza kundi la halmashauri za Manispaa kwa kukusanya asilimia 138 ya makisio huku Lindi ikishika nafasi ya mwisho kwa kukusanya asilimia 54 ya makisio.

Jafo alisema kwa upande wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeoongoza katika kundi la halmashauri za Manispaa kwa kigezo cha mapato ghafi baada ya kukusanyw Sh bilioni 58 huku Lindi  ikiwa ya mwisho kwa kukusanya Sh bilioni 1.0.

Aidha, JAfo alisema halmashauri ya Mji wa Geita imeongoeza kundi la halmashauri za miji kwa kigezo cha asilimia ambapo wamekusanya kwa asilimia 157 ya makisio huku halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya asilimi 11 ya makisio.

“ Katika kigezo ya pato ghafi kwa halmashauri za mji, Geita inaongeza baada ya kukusanya Sh bilioni 8.02 na halmashauri ya mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho ikiwa imekusanya Shilingi milioni 257.6.

Kwa upande wa halmashauri za wilaya, Jafo alisema Mbozi inaongoza kwa kukusanya kwa asilimia 171 ya makisio na ya mwisho ni Tandahimba iliyokusanya asilimia 19 ya makisio wakati kwa upande wa pato ghafi, Chalinze inaoongoza kwa kukusanya Sh bilioni 7.6 na ya mwisho katika kundi hili ni Gairo  iliyokusanya Sh milioni 396.1.

Aidha, Jafo aliwataka wakurugenzi ambao Halmashauri zao zimefanya vibaya katika ukusanyaji wa mapato kujitathimini na kuweka mikakati ya ya kuongeza vyanzo vya mapato na mapato ya halmashauri zao kwa ujumla.

Pia Waziri Jafo aliwaagiza Wakurugenzi ambao Halmashauri zao zimetoa mikopo ya wanawake, vijana na walemavu chini ya asilimia 50 kuandika barua za maelezo kwanini wasichukuliwe hatua kwa kuvunja sheria na barua hizo ziwasilishwe ndani ya muda wa wiki mbili.

Aliongeza kuwa Wakurugenzi wote wahakikishe  ukusanyaji wa mapato hayo ya ndani unaenda sambamba na upelekeji wa fedha kwenye miradi ya maendeleo na mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu.

Aidha, Mhe. Jafo ameendelea kusisitiza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.

(mwisho)



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.