• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Gwajima Asisitiza Uzalendo, Mapitio Ya Sera Ya Ugatuaji Wa Madaraka

Imewekwa tar.: December 10th, 2019

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, OR-TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wakurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara zote kutanguliza uzalendo katika kufanya mapitio ya Sera ya Kitaifa ya Ugatuaji wa Madaraka.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo mapema leo wakati wa kufungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Wizara zote wa Sera na Mipango  ambao wamekutana Jijini Dodoma kupitia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka na Programmu ya kuimarisha Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Dkt Gwajima amesema kuwa Wakurugenzi wote waliohudhuria kikao hiki ni wabobezi wa masuala ya mipango na bajeti katika Wizara zeo hivyo wanafahamu mahitaji ya wananchi halkadhalika mahitaji ya Wizara wanazofanyia kazi kwa upana wake kwahiyo wako katika nafasi nzuri ya kupitia Sera hii na kutoa mawazo yenye tija kwa manufaa ya Nchi yetu.

“Kazi hii ni nyeti sana kwa mustakabali wa Taifa letu, mnatakiwa mjitoe kwa dhati na muweke uzalendo mbele ili kulinda maslahi ya Nchi yetu, mjitume haswa katika kufanya kazi hii kwa weledi na moyo wote kwa sababu ninyi ndio wataalamu katika eneo hili; Makundi mengine yamepitia Sera hii lakini ninyi ni wataalamu na wabobezi wa Sera hivyo mchango wenu wenye ni muhimu sana kwa mafanikio ya Sera hii” alisisitiza Dkt. Gwajima.

Akizungumzia mafanikio ya Sera iliyokwisha muda wake Gwajima amesema Sera hiyo ilisaidia katika ongezeko la uelewa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo na utawala, iliongeza ari ya Wananchi katika kujitegemea kupitia upangaji wa Mipango na kuimarika kwa taratibu za kuwajibisha watumishi na viongozi katika ngazi husika.

Gwajima aliongeza kuwa Sera hii pia ilisaidia kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo Elimu, Afya, Maji, Miundombinu, biashara, makazi na ustawi wa jamii pamoja na kuimarika kwa uwajibikaji wa watumishi kwa kuwa wanasimamiwa katika ngazi ya msingi.


Wakati huo huo Gwajima alibanaisha changamoto za Sera hiyo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa mitazamo inayokinzana kati ya watendaji na viongozi wa kisiasa katika ngazi za vijiji, Kata na halmashauri katika kuweka vipaumbele na kutekeleza miradi ya maendeleo na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutegemea fedha kwa kiasi kikubwa kutoka Serikali Kuu.

Aliongeza kuwa Wizara za kisekta kutopeleka fedha zinazoendana na majukumu yaliyogatuliwa, mfumo hafifu wa mawasiliano kwa baadhi ya Wizara za Kisekta na OR-TAMISEMI pamoja kuwepo kwa Sera ya Ugatuaji iliyojengwa kwenye mfumo wa kisheria inayoelekeza mipaka, majukumu na utaratibu wa utekelezaji wake.

Naye Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta OR-TAMISEMI Dr. Andrew Komba amesema kuwa Sera iliyopo sasa ni ya mwaka 1998 hivyo imekwisha muda wake na kuna kila sababu ya kufanya mapitio ya Sera hiyo ili kuendana na mahitaji ya sasa na mabadiliko yaliyopo sasa.

“Tumehakikisha kuwa Sera ya sasa imefanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza katika utekelezaji wa Sera iliyokwisha muda wake na itajikita zaidi katika ujenzi wa uchumi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kujenga uchumi wa jamii na pia imejikita katika ushirikishwaji wa sekta binafsi pamoja na asasi zisizo za Kiserikali katika kutoa huduma bora kwa jamii.

Kwa kuwa sasa tunaelekea katika Uchumi wa Viwanda tumehakikisha Sera hii inajielekeza katika ushiriki kikamilifu katika ujenzi wa viwanda na inalenga maridhino ya makundi yote yaani Serikali, Sekta binafsi, Asasi zisizo za kiserikali, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa” alisisitiza Dr. Komba

Kikao hiki cha siku mbili kitapitia na kujadili rasimu ya Sera ya Ugatuaji wa madaraka kwa wananchi, mkakati wa utekelezaji wa Sera pamoja na Programu ya kuimarisha Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mwisho.


Matangazo

  • Badili Tahasusi kwa Wanafunzi Kidato cha Tano Tarajali na Vyuo vya Kati March 29, 2021
  • Kitabu cha Maombolezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. John Pombe Joseph Magufuli March 18, 2021
  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TARURA Iringa watumia shilingi milioni 153 kukarabati barabara za Kalenga

    April 12, 2021
  • Shilingi bilioni 1.5 zatumika kujenga vituo vinne vya afya Tunduru

    April 12, 2021
  • Waziri Ummy aanza na Sekretarieti za Mikoa

    April 12, 2021
  • Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais TAMISEMI akabidhiwa ofisi

    April 12, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.