• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Ep4r kukarabati Shule ya Ufundi ya Mwadui

Imewekwa tar.: March 11th, 2020

Na Ntenghenjwa Hoseah, Shinyanga

Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Gerald Mweli amesema kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo Serikali itakarabati shule ya Sekondari ya Ufundi ya Mwadui.

Mweli ameyasema hayo wakati alipotembelea Shule hiyo leo na kubaini uchakavu mkubwa wa miundombinu ambapo mpaka sasa shule hiyo imeshindwa kutoa Elimu bora ya Ufundi kutokana na uchakavu huo katika madarasa pamoja na karakana.

Akizungumza katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Mweli amesema amejionea uchakavu uliokithiri wa miundombinu ya Shule hiyo kitu ambacho kinaweza kupelekea hata wanafunzi kutofanga vizuri katika masomo kutokana na hali hiyo.

“Nimekuja hapa leo kujionea dhahiri ni kwa kiwango gani shule hii ni chakavu na jinsia ambavyo Serikali inaweza kuinusuru kwa kufanya ukarabati mkubwa utakaorudisha shule hii kwenye hadhi yake.

Elimu ya ufundi ni muhimu sana kwa watoto wetu haswa katika kipindi hiki ambacho Nchi inaelekea katika Uchumi wa Kati wa Viwanda ni lazima tuzalishe nguvu kazi yenye taaluma ya ufundi itakayosaidia katika viwanda vyetu” Alisema Mweli.

Aliongeza kuwa ufundi unasaidia kumjenga mtoto kuwa na Elimu ya kujitegemea sio lazima awe ameajiriwa  hivyo shule hii ikifanyiwa maboresho na kutoa Elimu ya ufundi kwa  wanafunzi wengi tutakua tumesaidia katika suala la ajira kwa vijana hao. 

“Sasa kwa hali hii kupitia  mradi wa lipa kutokana na matokeo “Ep4r” tutakarabati shule hii na kuirudisha kwenye hadhi yake na iendelee kutoa elimu ya ufundi wa watoto  wanaochaguliwa katika shule hii na kazi hiyo itaanza hivi karibu”

Akizungumza katika Shule hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe· Nyabaganga Taraba amesema Majengo mengi ya shule ya Ufundi Mwadui yamechakaa na 

mashine nyingi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo zimekufa hivyo shule haitoe elimu ile iliyokusudiwa hapo awali.

Shule hii ikikarabatiwa ni Mkombozi wa watoto wa Kishapu maana watapata ujuzi wa kutosha wa kuweza kuwasaidia katika maisha yao hapo baadae na ninaishukuru Serikali kwa kuona uchakavu uliopo na kuahidi kuikarabati nina uhakika kiwango chetu cha Elimu kitaongezeka baada ya ukarabati huo” alisema Taraba.

Naye Mkuu wa Shule ya Ufundi Mwadui amesema shule hiyo ilijengwa mwaka 1961 kwa ufadhili wa Mgodi wa Almasi wa Williamson na kwa  sasa ina wanafunzi 800; Elimu ya ufundi inayotolewa kwa sasa ni ujenzi, uselemala, umeme na kuchonga  vyuma.

Katika ziara hiyo pia Mweli alitembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadui ambayo pia iko kwenye hatua za ukamilishaji na itaanza kupokea wanafunzi hivi karibuni aliridhishwa na ukarabati unaoendelea na kumuagiza Mkuu wa Wilaya kuendelea na hatua za kuanza kutoa Elimu kwa watoto wa kike.



Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Tangazo la kazi kada ya Afya January 20, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Mweli awatega Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu kwenye Mfumo wa PREM/PREMS.

    January 10, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.