• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Dodoma lazidi kuwa Jiji la Mfano

Imewekwa tar.: May 9th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mhe.Selemani Jafo(Mb) amesema Serikali itaendelea kutenga fedha na kuelekeza miradi ya Kimkakati katika Jiji la Dodoma ili Jiji hilo liweze kuwa bora kama yalivyo majiji mengine ya Kimataifa.

Waziri Jafo aliyasema hayo katika  hafla ya utiaji saini mkataba wa ushauri katika utafiti na usanifu wa mfumo wa utiririshaji wa maji ya mvua na maandalizi ya mpango wa uboreshaji wa mifumo ya mitaro ya maji ya mvua na maji taka katika jiji la Dodoma kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2020 hadi 2040.

Jafo amesema kuwa Jiji la Dodoma linatakiwa kuendana na hadhi ya kamao makuu hivyo inahitaji fedha za kutosha za kuweza kuwekeza katika miundombinuyenye ubora itakayobadilisha sura ya Jiji.

“Hapa kunatakiwa kuwa na Maduka makubwa (Shoping Malls), Hoteli za hadhi ya nyota tano, majengo ya biashara, vivutio vya Utalii hata ikiwezakana patengenezwe bahari na fukwe za kupumzikia hii itafanya wananchi wa Jiji hili kupata huduma zote muhimu na kufurahia maisha wakati wote” Alisema Jafo.

Akizungumzia mkataba wa utafiti na usanifu amesema anachokitaka ni kuona mradi huu unajibu hoja za Wananchi wa Jiji hili kwa zaidi ya miaka ishirini ijayo kusiwe na changamoto katika eneo la maji taka na maji ya mvua.

Wakati huo huo, Waziri Jafo ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi makini katika matumizi ya mapato hayo.

“Jiji la Dodoma ndiyo Jiji pekee linaloongoza kwa ukusanyaji wa pato ghafi kwa Halmashauri zote nchini lakini kukusanya ni jambo moja na kutumia ni jambo linguine nafurahia leo kuona mnasini mkataba miradi ya maji katika kata ya Hombolo hongereni sana kwa hilo.

Akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema mradi huo utatoa suluhisho la kudumu katika kupambana na mafuriko ya mara kwa mara katika Jiji la Dodoma na utaweka mfumo thabiti wa ukusanyaji wa maji taka ili kuhakikisha mazingira ya jiji yanabaki kuwa nadhifu wakati wote.

Lengo la mradi huo ni  kuandaa mpango jumuishi wa mifumo ya maji ya mvua na maji taka  ambao utahusisha  mifumo ya maji ya mvua, ukusanyaji wa maji taka kutoka kwenye ngazi ya kaya, usafirishaji salama kutoka kwenye makazi, uhifadhi pamoja na uchakataji kwa lengo la kubadili maji taka kuwa bidhaa nyingine kwa matumizi anuai yenye tija na salama kwa jamii

Mradi utatekelezwa na mshauri msanifu toka kampuni ya Cheil Engineering Co. Ltd kutoka Jamhuri ya Korea Kusini kwa kushirikiana na kampuni ya AJOMA Consult Ltd. ya Tanzania kwa mkataba wenye gharama ya Shilingi 1,575,573,813.10, ambao utatekelezwa kwa muda wa miezi 12 kuanzia tarehe Mei 6, 2019 mpaka Mei 5, 2020.

Aidha Mradi huu uko chini ya mradi mama wa Uendelezaji wa Miji Mkakati  (TSCP) awamu ya pili unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.


Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.