• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

DMDP Waipongeza Serikali, Usimamizi mzuri wa Miradi

Imewekwa tar.: May 22nd, 2019

Mtaalam wa Mipangomiji na msimamizi wa mradi wa DMDP Erick Dickson, amepongeza mwenendo wa utekelezaji wa mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP) unaosimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI).

Erick ametoa pongezi hizo tarehe 20 Mei, 2019 mara baada yakurejea nchini, wakati wa mkutano mkuu wa tathimini ya mwaka ya Miradi ya  DMDP,  Mradi wa Uimarishaji Halmashauri za Miji (ULGSP) na Mradi wa Uimarishaji Halmashauri za Miji ya Kimkakati (TSCP) unaofanyika kwa siku tano Jijini Dar es Salaam .

“Mtazamo wangu na wa timu ya Benki ya Dunia ni kuwa DMDP ipo kwenye mwelekeo sahihi na kazi nyingi zinaendelea kutekelezwa vizuri. Pongezi nyingi ziende kwa timu nzima inayosimamia mradi wa DMDP na wote wanaofanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kuwa DMDP inaleta mafanikio na mabadiliko makubwa. Huu Ndiyo ujumbe tutakao anza nao katika mkutano huu,” alisema Erick.

Ndugu Erick alieleza kuwa, mradi unatekelezwa katika mazingira ambayo kazi nyingi zinafanyika kwa pamoja ikiwepo, Kupandisha hadhi makazi yaliyopangwa kiholela, ujenzi wa barabara zinazounganisha barabara za mwendokasi na barabara kuu (feeder roads), barabara za Mitaa pamoja na mifereji ya maji ya mvua, masoko, vituo vya daladala na nyinginezo.

“ Pamoja na hayo yote taarifa ninazopata ni kwamba tuna mradi ambao tunafanya vizuri na kuleta mabadilliko makubwa pamoja na kuwepo kwa changamoto za kawaida hili ni  jambo la kujivunia,” alisisitiza.

Naye Mratibu wa Kikundi kazi cha utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia (WBWG) Mhandisi, Davis Shemangale alisema kwamba, mradi wa DMDP unatekelezwa ukienda sambamba na Mpango Makakati wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini ifikapo 2025.

“kwa kuzingatia kuwa Dar es Salaam inachangia sehemu kubwa ya pato la Taifa, DMDP hadi sasa imewezesha kwa kiasi kikubwa kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji na kuongeza mawasiliano na muunganiko wa bararabara kwa maeneo ambayo yalikuwa ni vigumu kufikika hapo awali, hali hiyo imeongeza uimarikaji wa shughuli za kiuchumi” alisema Shemangale.

Mhandisi Shemangale alisema, madhumuni ya Mkutano huo ni kufanya mapitio na kutoa tathmini ya mradi ulipofikia katika utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu, maswala ya matumizi ya fedha na utekelezaji wa maswala ya kimazingira na usalama kama yanatimiza vigezo vya kimataifa vilivyoainishwa. Shemanagale  alieleza kuwa, mradi wa DMDP hadi kufikia takribani ni nusu ya utekelezaji wake tayari umekukumbana na changamoto mbalimbali, ukiwapo msongamano mkubwa uliopo katika Jiji ambapo ni takribani ni asilimia 80 ya makaazi yamejengwa kiholela.

“Jiji ni kubwa na linamsongamano Mkubwa na changamoto mojawapo ni upatikanaji wa malighafi za ujenzi katika naeneo ya mbali na mji. Pia ulipaji fidia umekuwa na changamoto mbalimbali zilizosababisha utekelezaji wa mradi kuchelewa katika baadhi ya maeneo,” alisema Mhandisi Shemangale.

Katika hatua nyingine aliishukuru Benki ya Dunia na hasa kiongozi wa timu ya Mradi Erick Dickson kwa kushirikiana kikamilifu na Serikali na kufanya kazi bila kuchoka, ili kuhakikisha changamoto zote za mradi zinashughulikiwa ili kuhakikisha mradi unatekelezwa na kukamilika katika ubora uliokusudiwa.

Mradi wa DMDP unatekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa gharama ya shilingi bilioni 660, ambazo ni mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia, huku serikali ikichangia shilingi bilioni 25 kama sehemu ya mchango wa serikali.

Anaandika Rapahael Kilapilo- TAMISEMI-DSM.

Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.