• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Dkt Gwajima awabadilikia CHMT Chamwino, awapa siku saba kujieleza

Imewekwa tar.: August 28th, 2019

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima  ametoa siku saba kwa  Timu ya uendeshaji  huduma ya afya Wilaya  CHMT  katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kujieleza  kwa kushindwa kutimiza wajibu wao licha ya kupatiwa maelekezo.

Ameyasema hayo leo alipowaita timu hiyo ofisini kwake mara baada ya ziara yake ya kutembelea katika zahanati ya Chiboli iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoani Dodoma kujionea utoaji wa huduma za afya katika Halmashauri hiyo.

Amewataka timu hiyo kujieleza kwa nini wasitolewe kwenye majukumu yao ya uongozi kwa kushindwa kutimiza wajibu licha ya maelekezo na msaada ambao wamekuwa wakipewa.

Dkt Gwajima amesikitishwa na hali aliyoikuta  katika zahanati hiyo ambapo hakukuwa na kitanda cha kujifungulia wala kitanda cha kupumzika baada ya mama kujifungua huku kukiwa na rekodi za mfululizo wa ziara za CHMT hao katika kituo hicho.

“Haiwezekani mkawa mnafanya ziara za usimamizi wa kitalii huku mnalipana posho halafu hakuna mabadiliko hata yaliyo wazi” Amesema Dkt. Gwajima.

Anafafanua kuwa Zahanati ya Chiboli iliyopo Halmshauri ya Wilaya ya Chamwino imebainika kufanya vizuri katika kutoa huduma kwa wanachama wa CHF iliyoboreshwa licha ya kuwa na upungufu mkubwa wa watumishi.

Dkt. Gwajima amesema wananchi wamekiri kuridhishwa na nidhamu ya watumishi wa kituo hicho licha ya kuwapo wawili  katika kituo kizima jambo ambalo ni nadra sana kukuta katika vituo vingine vya kutolea huduma.

“Inakuwaje watumishi hawa wako wawili tu wanakubalika na jamii na wamesimamia uhamasishaji wa CHF iliyoboreshwa hadi mwitikio sasa uko juu halafu hawapewi msaada na wasimamizi katika kuboresha zaidi huduma? hivi kweli kitanda cha kujifungulia nacho kiwe shida wakati fedha zipo na bila shaka kwenye vituo vingine vipo vya ziada?” Amehoji Dkt Gwajima.

Amewaagiza CHMT kuhakikisha kitanda kinapatikana  na kuhakikisha kimefika na watume picha wakiwa na watumishi wa kituo hicho wakiwa wanapokea hicho kitanda cha kujifungulia vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Vilevile, ameziagiza CHMT zote nchini kufanya sensa ya vifaa na uwiano wake kila kituo ili kufanya uhamisho wa vifaa vilivyozidi toka kituo kimoja kwenda kituo chenye upungufu na sio muda wote kuwaza kununua.

 “Nafahamu fika kuwa katika baadhi ya vituo kuna ziada ya vifaa na kwingine pungufu shida ni kuwa, hatutaki kufanya uchambuzi wa raslimali bali mara zote tunawaza kununua tu” Amesema Dkt. Gwajima.

Dkt Gwajima amesema asiyeenea kwenye kiti cha uongozi wa CHMT au RHMT na ambaye anajihisi kuwa yeye amekuwa sugu hataki kubadilika kwa maelezo ya kawaida basi afahamu fika hatachwa apumzike kwenye kiti hicho bali atampangiwa kiti kinachomtosha.

Aidha, amewapongeza watumishi wa Zahanati ya Chiboli akiwemo Muuguzi Shija Makeja na Mtaalamu wa Maabara Bw. Waziri Mkemangwa ambao licha ya uchache wao na kuwa mbali na mjini kwa kilometa zaidi ya 90 wameonesha umahiri mkubwa wa kazi na uzalendo mkubwa kiasi kwamba wamevishinda vituo vingine vyenye watumishi wengi na vilivyoko mjini kwa kusimamia uhamasishaji wa CHF iliyoboreshwa.

Dkt. Gwajima amesema, watumishi hawa wanastahili kutiwa moyo na kusaidiwa na CHMT yenye uwajibikaji na siyo hawa ambao wao ziara za usimamizi ni kwenda kupumzika.

Dkt. Gwajima amewashukuru viongozi wa Kamati ya Usimamizi wa Kituo inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji Ndg. Ernest Mgona pia amemshukuru Mtendaji wa Kijiji Ndg. Lucas Gideon kwa kuwapa ushirikiano wa kutosha wataalamu hadi kupata mafanikio makubwa kuhusu CHF Iliyoboreshwa.

Dkt. Gwajima ameagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kupitia Idara ya Afya apeleke watumishi wengine wawili akiwemo tabibu na kama hawapo ahamishe hao wataalamu wa CHMT wakafanye hapo.

Amefafanua kuwa ufuatiliaji uliofanywa na OR TAMISEMI umebaini kuwa tayari kitanda hicho kimeshafika na pangua pangua ya vifaa vilivyozidi katika vituo mbalimbali inaendelea ili kuweka uwiano sahihi wa vifaa na huduma.

Aidha  Kijiji cha Chiboli kina wakazi 5357 na Kaya 500 ambapo, kuanzia Januari, 2019 jumla ya Kaya 315 sawa na 63% zimejiunga na mfuko wa CHF iliyoboreshwa na wamekiri kufurahia kuwa wanachama wa mfuko huo kwani sasa wanaweza kupata huduma hadi hospitali ya rufaa ya mkoa na katika mkoa wowote ule tofauti na awali ambapo, walikuwa wanapata kwenye kituo hicho tu walikojiandikisha.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI




Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.