• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu

Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

Imewekwa tar.: January 22nd, 2021

Na Atley Kuni, Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, amesema uwekezaji wa sh. bilioni 16.4 zilizotumika kukarabati shule 9 za ufundi nchini imezifanya shule hizo kurejea katika hadhi yake.

Ameeleza kumalizika kwa kazi hiyo ya kukarabati shule hizo zilizokuwa na miundombinu chakavu kutawezesha wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na shule hizo kuhitimu wakiwa na ujuzi uliokusudiwa na Serikali.

Mbali na uwekezaji wa fedha hizo, Serikali pia imeajiri walimu 150 ambao wamepangwa katika shule zote 9 lengo likiwa ni kupata tija iliyokusudiwa kwa Watoto wa kitanzania kuhitimu wakiwa na maarifa yakuweza kujiajiri.

Waziri Jafo, amesema lengo la Serikali ya awamu tano, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, ni utekelezaji sera ya Tanzania ya Viwanda iliyo asisiwa mwaka 2016, ambapo amesema wanafunzi hao baada ya kuhitimu elimu zao wataweza kujiajiri katika viwanda vidogo, lakini vile vile kutumika katika viwanda mbalimbali hapa nchini.

“Hatutegemei kuona, wanafunzi wakiwa shuleni wanajifunza nadharia peke yake, tunataka wajifunze pia kwa vitendo ili wawe na ujuzi wakuzalisha baadhi ya vitu wanavyo jifunza mathalani chaki, Vijiti vya kusafisha kinywa ‘toothpick’, kwakutaja baadhi, na kuongeza kuwa,

“katika wakati wa sasa ni vema kufikiria zaidi nje ya boksi, na hasa kwakuwashirikisha baadhi ya wataalam mafundi wa mtaani wenye maarifa ya kutosha katika fani tofauti tofauti ili  kuwaongezea maarifa na ujuzi wanafunzi hao”.

Shule zilizokarabatiwa na ambazo tayari zimesha pangiwa wanafunzi na walimu wa fani mbalimbali ni Bwiru wavula ya mkoani Mwanza iliyo fanyiwa ukarabati kwa gharama ya Zaidi ya sh. Milioni 825, Shule ya Ufundi Chato ya mkoani Geita iliyokarabatiwa kwa gharama ya shilingi bilioni 3.9, Shule ya Ufundi Ifunda ya mkoani Iringa kwa gharama ya shilingi bilioni, 3.6, Shule ya Ufundi Iyunga iliyopo mkoani Mbeya iliyo gharimu shilingi bilioni 1.01 na Moshi Ufundi ya mkoani Kilimanjaro iliyokarabatiwa kwa shillingi bilioni 2.1.

Shule zingine ni Shule ya Ufundi Mtwara, kwa gharama ya bilioni, 1.3 Musoma ufundi ya mkoani Mara, kwa gharama ya shilingi bilioni 1.2 Mwadui ya mkoani Shinyanga, iliyo pokea milioni sh. Milioni 226 kwa ajili ya ukarabati na Shule ya Ufundi Tanga ya mkoani Tanga, iliyo gharimu shilingi, bilioni 2.1 ambapo gharama yake kuu ni sh. bilioni 16,4.

Wakiongea kwa njia ya Mkutano kwa masafa ‘Video Conferences’ wakuu wa mikoa hiyo pamoja na wataalamu walioshiriki kikao hicho, kutoka katika Mikoa hiyo tisa, waliiomba Serikali kuhakikisha inaboresha Mitaala ili iweze kukidhi mahitaji ya sasa, ambapo Waziri Jafo, akitolea ufafanuzi alisema, anaipongeza Wizara ya Elimu kwa kazi kubwa ya maboresho ya Mitaala lakini akautaka uongozi wa Elimu TAMISEMI, kulichukua jambo hilo na kulifanyia kazi kama ilivyo shauri.

Akihitimisha kikao hicho, Waziri Jafo, amewaelekeza Wakuu wa Mikoa kuwa walezi wakuu shule hizo, kwakuzitembelea na kujua changamoto wanazokabiliana nazo lakini pia kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Katika hatua nyingine, Waziri jafo ametumia wasaa huo, kuwagiza Wakurugenzi kuhakikisha wanawalipa fedha za kujikimu watumishi wote waliopangiwa kazi katika maeneo yao ndani ya siku saba.

 

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali yalegeza masharti mikopo ya asilimia 10

    February 27, 2021
  • Vikundi 23 Wilayani Busega vimenufaika na mikopo ya asilimia 10

    February 26, 2021
  • Vikundi 366 Wilayani Kilwa vyanufaika na mikopo ya sh bilioni 1.1

    February 26, 2021
  • Waziri Jafo ataka Zimamoto, Skauti wakomeshe majanga ya moto shuleni

    February 26, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.