• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Astashahada, Stashahada Msizipe Kisogo: Waziri Jafo

Imewekwa tar.: April 18th, 2018

Kuashiria kuwasili, Mhe. Waziri akisaini kitabu cha wageni.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuanza kwa kozi za ngazi ya Shahada katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kisiwe kigezo cha kuondosha kozi za Astashahada na Stashahada katika chuo hicho.

Waziri Jafo alikuwa akizundua rasmi Bustani ya  Magufuli katika chuo hicho ambapo Bustani hiyo itatumika kuishi na kuenzi mchango wa kiongozi huyo wa Nchi kwasasa ambao ni uzalendo, kujituma pamoja na uadilifu katika kuwatumikia wananchi.

“Nimesikia maombi yenu yakutaka Kuanzishwa kwa kozi za Ngazi ya Shahada kusudi mtu anapo hitimu masomo yake ya ngazi za awali aweze kuendelea, naomba niwambie, tutajitahidi lifanikiwe, lakini angalizo langu kwenu, tutakapo anzisha Degree isiwe sababu yakusitisha kozi zinazoendelea kwa sasa, ikiwepo Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) ya kozi mnazo endelea nazo” amesema Jafo.

Waziri Jafo amesema, vyuo vingi vilipo anzisha ngazi ya Shahada na kusahau wataalam wa kada za kati vilichochea kukosekana kwa wataalam wakutosha katika ngazi ya kati hususan mafundi mchundo ambao walikuwa wakizalishwa katika vyuo hivyo.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo amewahakikishia Wakurufunzi hao wa chuo cha Hombolo uhakika wa kuajiriwa na Serikali kwa wale watakao fikia vigezo vinavyo hitajika katika nafasi mbali mbali ambazo serikali itatangaza.

“Tumebaini Wataalam wa chuo cha Hombolo  tunaowaajiri katika kada za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na hata Tarafa wanauelewa mpana wa Masuala ya jamii za watanzania hususan ni wale waishio vijijini, hivyo basi tunapotangaza ajira kipaumbele tutakitoa kwa  wanafunzi wa chuo hiki” amesema Waziri Jafo.

Mhe. Jafo hakusita kuonesha furaha yake kwa jinsi chuo hicho kilivyo jizatiti katika suala la utunzaji wa mazingira, hatua ambayo ameitaja ni  kumuunga mkono Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye kupitia Wizara ya Mazingira na Muungano amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania wanantunza mazingira.

Mbali ya pongezi hizo Waziri  ametoa maelekezo kwa uongozi wa Manispaa ya Dodoma kuanza kampeni ya upandaji wa miti ya Matunda. “Tunataka Dodoma iwe Fruit City” amenukuliwa Waziri

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi inayomaliza Muda wake Prof. Suleiman Ngware, yeye alisema lengo la kujenga Bustani ya  Magufuli nikuunga mkono juhudi za Mhe. Rais katika kusimamia rasilimali za nchi kwa moyo uzalendo na uadilifu wa dhati.

“Mhe. Waziri Shabaha yakuwa na Bustani ya aina hii yenye Mnara wa Magufuli nikutambua mchango mkubwa na moyo wa kizalendo alionao Rais wetu, sasa tunachotaka nini hapa, kila mtu atakaye uangalia mnara huu aweze kujitathmini mwenyewe bila yakusukumwa na mtu, Je! Mimi kama Mkufunzi ninatimiza wajibu wangu? Mimi kama Mwanafunzi nafanya matendo sawa na Rais wangu? Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi au Mkuu wa Shule sifanyi manyanyaso kwa watu sibagui watu nk, nk". Amesema Mwenyekiti huyo.

Kila Mwaka ifikapo Aprili 18, Bodi, Uongozi, Wanafunzi na Wananchi wanaozunguka eneo la chuo watakuwa wakikutana kwa pamoja na kujitathmini kwa mienendo na matendo yao ya utendaji wa mwaka mzima, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kwa sasa kinawanafunzi zaidi ya 3000.

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo akisema neno wakati wa Hafla hiyo.

Bodi ya Chuo iliyomaliza muda wake

Hii ndio Magufuli Square 

Kikundi cha Ngoma cha Swala ambacho hupatikana Kijiji cha Nkoyo  Hombolo



Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Tangazo la kazi kada ya Afya January 20, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Mweli awatega Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu kwenye Mfumo wa PREM/PREMS.

    January 10, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.