Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Historia ya Taasisi

1.1    Utangulizi
Nchi  yetu ilipata Uhuru Tarehe 09.12.1961 ambapo Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza aliunda Wizara ya Serikali za  Mitaa na Kumteua Mhe. Job Lusinde kuwa Waziri wa kwanza kuongoza Wizara  hii. Akifuatiwa na Mawaziri 19 ikijumuisha wanawake watatu (3) akiwemo  Waziri wa sasa Mhe. Ummy Mwalimu.

Tangu mwaka 1961 hadi sasa  Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea, Wizara chini  ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kwenye Ofisi ya Rais kama ilivyo sasa. Uamuzi  wa wapi inawekwa umekuwa ukifanyika ili kuimarisha utendaji wa Ofisi  hii.

Ofisi ya Rais TAMISEMI ni Wizara pekee ambayo Makao Makuu  yake yalianzia Jijini Dodoma tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini tangu  Serikali ilipotangaza Makao Makuu ya Serikali kuwa ni Dodoma na kwa Dar  es salaam kumekuwa na Ofisi ndogo. Uwepo wa Makao Makuu Dodoma ulikua na  lengo la kutoa fursa sawa kwa wadau wake wakuu hususan Mikoa na Mamlaka  za Serikali za Mitaa kufika Dodoma kwa urahisi wanapofuata huduma  mbalimbali.

Madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka  Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika Sura ya 8, Ibara ya 145 na  146. Upelekeaji wa madaraka kwa wananchi unapitia katika Mamlaka za  Serikali za Mitaa na ndiyo maana Serikali za Mitaa na ushirikishwaji wa  Wananchi katika mchakato wa maendeleo vimetambuliwa katika Katiba na  Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Wakati Nchi yetu inapata  uhuru wake kulikuwa na majimbo kumi ya Utawala ambayo yaliritihiwa toka  utawala wa kikoloni wa Kiingereza mwaka 1966. Rais wa kwanza Hayati  Julius Kambarage Nyerere kwa Mamlaka aliyopewa aliunda Mikoa 15 na  kuondoa utaratibu wa mgawanyo wa nchi katika Majimbo. Hadi Sasa Nchi  yetu ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956,  Vijiji 12,319, Vitongoji 64,384 pamoja na Mitaa 4,263. Baada ya uhuru  Halmashauri zilikuwa jumla 45 na hadi kufikia mwaka 2009 zilikuwa  Halmashauri 129 na zimeendelea kuongezeka hadi kufikia 184 mwaka 2021.

Wakati  wa Uhuru hakukuwa na Halmashauri za Majiji na sasa kuna Halmashauri za  Majiji 6, kulikuwa na Halmashauri ya Manispaa moja ya Dares Salaam na  sasa kuna Halmashauri za Manispaa 20, Halmashauri za Miji zilikuwa 9 na  sasa Halmashauri za Miji ni 21 na Halmashauri za Wilaya zilikuwa 10 na  sasa zipo Halmashauri za Wilaya 137.

Serikali iliendelea na  mfumo wa Serikali za Mitaa uliorithiwa kutoka kwa Wakoloni na kuutumia  kama nyenzo za kuleta maendeleo kwa misingi ya Kidemokrasia. Kutokana na  changamoto mbalimbali zilizoukabili utendaji wa Mamlaka za Serikali za  Mitaa baada ya uhuru mwanzoni mwa miaka ya sabini, Serikali ilifuta  Mamlaka hizi na kuanzisha mfumo wa Madaraka Mikoani.

Mfumo huu  ulizifanya Serikali za Mitaa kuitegemea Serikali Kuu kwa kila jambo  kutokana na wananchi kutoshiriki katika maamuzi na pia katika shughuli  za maendeleo, uchumi wa nchi ulididimia na viwango vya maisha kushuka.  Kutokana na hali hii, Serikali za Mitaa kwa upande wa Mamlaka za Miji  zilirejeshwa tena mwaka 1978 na mwaka 1984 Serikali za Mitaa  zilirejeshwa upande wa Mamlaka za Wilaya pia zilirejeshwa.

Kwa  lengo la kuziimarisha Serikali za Mitaa na kuziwezesha kutoa huduma bora  kwa wananchi, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali. Mojawapo ya  hatua hizi ni kuanzishwa kwa Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali  za Mitaa ulioanzishwa mwaka 1998 ambao ulilenga katika kupeleka madaraka  kwa Wananchi (D by D).

Katika kipindi hicho cha Maboresho,  Serikali ilitoa Tamko la Kisera la Ugatuaji wa Madaraka- Policy Paper on  Local Government Reform Programme on Decentralization by Devolution  (D-by-D) kama njia muafaka ya kufikisha na kuharakisha maendeleo ya  Kijamii na Kiuchumi na kuinua utoaji wa huduma kwa wananchi. Uamuzi huu  wa kisera umelenga kuondokana na mapungufu yaliyokuwepo katika Mifumo ya  awali na kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizokuwepo.

Dhana hii  ya D by D imejengwa kwa misingi ya kutoka kwenye mfumo wa Madaraka ya  Serikali Kuu kuwa na maamuzi yote na Serikali za Mitaa kuwa Mtekelezaji  tu (yaani Mwagizaji na Mtekelezaji) kwenda katika mfumo wa Serikali za  Mitaa wenye Mamlaka ya Kisheria ya kuamua mambo katika eneo lao na  kuyatekeleza. Hivyo, kuwa na mfumo wa mahusiano ya majadiliano katika  utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Dhana hii inalenga kupeleka  madaraka zaidi kwa wananchi.

Dira

Kuwa Taasisi inayoongoza katika kuwezesha Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa  kwa  kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dhima

Kutengeneza mazingira wezeshi ya utekelezaji wa Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma, Maendeleo Vijijini na Mijini, Sheria, Miongozo na Viwango ili kuiwezesha Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa huduma bora kwa wananchi na kuondoa umaskini.


Majukumu ya OR-TAMISEMI

Majukumu ya OR-TAMISEMI yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais  Aprili 2016, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-
i)    Kuratibu utekelezaji wa Sera ya  Maendeleo  Mijini na Vijijini  na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii)    Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii)    Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv)    Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri  kutekeleza wajibu wake;
v)    Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi)    Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi; na
vii)    Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI.


Muundo wa OR-TAMISEMI
Kwa mujibu wa Muundo uliopitishwa na Kamati ya Utekelezaji (Presidential Implementation Committee-PIC) Mwaka 2017, OR-TAMISEMI ina jumla ya  Idara 11 na Vitengo 6 vyenye jumla ya Wakurugenzi 11, Wakurugenzi Wasaidizi 25 na Wakuu wa Vitengo 6. Pia Ofisi inasimamia Taasisi saba (7) zilizopo chini yake.

Idara 11 zilizopo ni kama ifuatavyo:-
1)    Idara ya Utawala na Rasilimali Watu;
2)    Idara ya Sera na Mipango;
3)    Idara ya Teknolojia Habari na Mawasiliano;
4)    Idara ya Huduma za Sheria;
5)    Idara ya Maendeleo ya Miundombinu;
6)     Idara ya Tawala za Mikoa;
7)    Idara ya Serikali za Mitaa;
8)    Idara ya Uratibu wa Sekta;
9)    Idara ya Usimamizi wa Elimu;
10)    Idara ya Maendeleo ya Miji; na
11)    Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe.

Vitengo sita (6) vilivyopo ni kama ifuatavyo:-
1)    Kitengo cha Uhasibu  na Fedha;
2)    Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani;
3)    Kitengo cha Mawasiliano  Serikali;
4)    Kitengo cha Ununuzi na Ugavi;
5)    Kitengo cha Huduma za Kimenejimenti; na
6)    Kitengo cha Ukaguzi na Ufuatiliji  wa Matumizi ya Fedha.

Taasisi saba (7) zilizopo ni kama ifuatavyo:-
1)    Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC);
2)    Shirika la Elimu Kibaha (KEC);
3)    Chuo Cha Serikali za Mitaa, Hombolo (LGTI);
4)    Wakala wa Usafiri wa Haraka Dar es Salaam (DART);
5)    Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa (LGLB);
6)    Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA); na
7)    Shirika la Masoko Kariakoo.

Majukumu ya Idara

Idara ya Utawala na Rasilimali Watu:-

i)    Kutafsiri Sheria za Kazi, utumishi wa Umma, na Kanuni za Kudumu za Utumishi;
ii)    Kusimamia na kuendeleza mahusiano bora kazini na ustawi wa watumishi kazini katika masuala ya afya, usalama, michezo na Utamaduni;
iii)    Kusimamia uboreshaji na utoaji wa huduma bora za masjala na utunzaji wa Kumbukumbu za Ofisi;
iv)    Kuratibu na kusimamia shughuli zinazotolewa na makampuni ya watu binafsi ( Usafi na Usalama);
v)    Kuratibu mapambano dhidi ya rushwa mahala pa kazi;
vi)    Kuratibu mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mahala pa kazi;
vii)    Kusimamia masuala yote yanayohusiana na rasilimaliwatu ikiwemo ajira, kuthibitishwa kazini/cheo,kupandishwa vyeo, uhamisho, nidhamu, kustaafu, maslahi na mafunzo;
viii)    Kuratibu na kusimamia mfumo wa kutathmini na kupima utendaji Kazi kwa Uwazi kwa watumishi wote  (OPRAS);
ix)    Kuandaa Ikama ya watumishi na mishahara, Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na maendeleo (PE, OC & Dev);
x)    Kuratibu uandaaji wa maelezo ya kazi (JDs) kwa watumishi katika Idara na Vitengo;
xi)    Kuratibu uandaaji wa Mpango wa Mafunzo kwa kuzingatia Taarifa ya Tathmini juu ya mahitaji ya mafunzo (TNA); na
xii)    Kuratibu na kusimamia Mipango ya kurithishana Kazi na mafunzo ya awali.

Idara ya Sera na Mipango:-
i)    Kuratibu uandaaji wa nyaraka za Baraza la Mawaziri zinazotayarishwa na OR-TAMISEMI na Taasisi zake;
ii)    Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sera za OR-TAMISEMI na Sera za kisekta;
iii)    Kuchambua na kutoa maoni kuhusu Nyaraka za Baraza la Mawaziri (BLM) zinazoandaliwa na Wizara zingine;
iv)    Kuratibu uandaaji wa Bajeti na Mipango ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mikoa na Halmashauri;
v)    Kufanya Ufuatiliaji na Tahmini kuhusu Mipango na Bajeti na kuandaa tarifa ya utekelezaji wake katika ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI;
vi)    Kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu mipango ya Ofisi ya Rais- TAMISEMI ili kupata taarifa zitakazosaidia katika kufanya maamuzi kwa manufaa ya siku za baadaye;
vii)    Kuratibu maandalizi na mapitio ya Mpango Mkakati wa OR - TAMISEMI;
viii)    Kuhuisha mipango na bajeti ya OR - TAMISEMI katika mfumo na mchakato wa bajeti ya Serikali;
ix)    Kuratibu na kuandaa majibu ya hoja za Waheshimiwa Wabunge zinazohusu ngazi zote za TAMISEMI (OR - TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
x)    Kuandaa taarifa za utekelezaji zinazowasilishwa kwenye Mamlaka mbalimbali.

Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano:-
i)    Kutoa msaada wa kiufundi, kitaalam na kushauri masuala yanayohusu TEHAMA kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) na kusisitiza matumizi sahihi ya masuala ya TEHAMA na kufuatilia utekelezaji wake;
ii)    Kuchambua huduma za kielektroniki na kuwezesha matumizi ya Serikali Mtandao katika Sekretarieti za Mikoa na MSM;
iii)    Kutengeneza na kukarabati miundombinu na mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA);
iv)    Kuratibu masuala ya takwimu za kisekta katika Sekretarieti za Mikoa na MSM;
v)    Kuandaa Mkakati mpana wa TEHAMA na Mpango wa Utekelezaji;
vi)    Kuandaa Miongozo, Maelekezo na Machapisho ya uendeshaji wa masuala ya TEHAMA kwenye Sekretarieti za Mikoa na MSM;
vii)    Kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi katika masuala ya TEHAMA na Takwimu waliopo kuanzia ngazi ya kituo hadi Wizara.

Idara ya Huduma za Sheria:-
i)     Kutoa ushauri na utaalamu wa kisheria kwa OR-TAMISEMI, Taasisi zilizo chini yake, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
ii)    Kupitia na kuchambua  Sheria Ndogo za Halmashauri kabla ya kuidhinishwa na Waziri;
iii)    Kuandaa na kupitia nyaraka mbalimbali za kisheria kama vile mikataba, MoU na hati za kisheria;
iv)    Kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuandaa Miswada mbalimbali ya kutunga Sheria na au kurekebisha sheria zilizopo;
v)    Kuandaa Kanuni na Taarifa mbalimbali na Sheria Ndogo za mfano zinazotolewa na Waziri
vi)    Kuendesha kesi mahakamani zinazohusu Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri;
vii)    Kuratibu zoezi la kuhuisha Sera na Sheria za kisekta ili ziendane na Dhana ya Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma (Legal Harminisation Task Force); na
viii)    Kuchambua nyaraka na miswada mbalimbali ya kisheria.

Idara ya Maendeleo ya Miundombinu:-


i)    Kutambua mipango na kuratibu mgao wa rasilimali za Taifa kwa ajili ya matengenezo na maendeleo ya miundombinu;
ii)    Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa atika nyanja zote zinazohusiana na miundombinu na majengo;
iii)    Kufuatilia uzingatiaji wa viwango vilivyowekwa kuhusu ujenzi na ubunifu wa majengo;
iv)    Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya matengenezo na maendeleo ya miundombinu ya mijini na vijijini katika MSM;
v)    Kuandaa na kutumia mikataba ya utekelezaji wa kazi za miundombinu katika MSM;
vi)    Kuchambua na kuunganisha taarifa za utekelezaji kutoka Sekretarieti za Mikoa na MSM;
vii)    Kufanya tafiti za teknolojia sahihi kuhusu miundombinu ya barabara na nyumba katika MSM;
viii)    Kuwezesha na kuratibu pembuzi yakinifu na kuangalia athari za miundombinu katika MSM;
ix)    Kuandaa mahitaji ya mafunzo kwa wahandisi wa Sekretarieti za Mikoa na MSM kuhusu maendeleo ya miundombinu;
x)     Kuimarisha mfumo wa kusimamia na kudhibiti takwimu katika MSM;
xi)    Kuratibu uanzishwaji wa maabara za upimaji wa ubora wa kazi za barabara katika Sekretarieti za Mikoa na MSM; na
xii)    Kuchambua na kuunganisha taarifa za tafiti za miundombinu kutoka Sekretarieti za Mikoa na MSM.

Idara ya Tawala za Mikoa:-
i)    Kuratibu, Kusimamia, Kuzijengea uwezo wa kitaalam Sekretarieti za Mikoa ili ziweze kutoa ushauri, kuziwezesha na kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutekeleza majukumu/wajibu wake;
ii)    Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mipango na Bajeti katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, na
iii)    Kufuatilia na kuratibu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kama vile masuala ya Ulinzi na Usalama, Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii na masuala mtambuka.

Idara ya Serikali za Mitaa:-
i)    Ili kufanikisha lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi, Idara inatekeleza yafuatayo; - Kusimamia na kuendeleza utawala bora katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
ii)    Kujenga uwezo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutekeleza majukumu yake;
iii)    Kufuatilia utendaji wa Wakurugenzi na Wakuu wa Idara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
iv)    Kufuatilia matumizi ya fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
v)    Kufanya ukaguzi wa hali ya utoaji huduma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
vi)    Kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya utoaji huduma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Idara ya Uratibu wa Sekta:-
i)    Kuwa kiungo kati ya Wizara za Kisekta, Mikoa, Halmashauri, Idara za Serikali, Wakala, Wadau wa Maendeleo na Mashirika yasiyo ya Kiserikali (Non-State Actors (NSAs);
ii)    Kupokea taarifa/takwimu mbalimbali kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) kuzichambua na kuziwasilisha kwenye Wizara za Kisekta na Wadau wa Maendeleo;
iii)    Kushiriki katika utungaji na mapitio ya Sera na Miongozo ya Wizara za Sekta;
iv)    Kusimamia na Kufuatilia utekelezaji wa programu za Maendeleo (M &E) kwa kushirikiana na Wizara za kisekta;
v)    Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa matokeo makubwa (BRN) katika sekta ya Kilimo na Maji;
vi)    Kuratibu, kusimamia na kutekeleza mkakati wa Sekta ya Maji , Kilimo na Mazingira kwa kushirikina na Wizara za Kisekta katika kuratibu na kutekeleza shughuli za Miradi na Programu za Kisekta katika Mikoa na MSM;
vii)    Kwa kushirikiana na Wizara za Sekta ya Kilimo kuandaa, kupitia, kuboresha, na kusambaza Miongozo na Sera kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
viii)    Uratibu wa Sera ya upelekaji wa Madaraka kwa wananchi (D by D) na utekelezaji wake katika Wizara za Kisekta.

Idara ya Uendeshaji na Usimamizi wa Elimu:-
i)    Kutoa mafunzo ya Walimu 50,446  walioko kazini kwa kuzingatia mtaala mpya (K.K.K) kwa walimu wa Darasa la I na II;
ii)    Kukuza ushirikiano wa shule na jamii kupitia kamati za shule;
iii)    Kutoa Elimu ya uongozi na Mipango (Education Grant for Management and Planning) kwa watendaji wa halmashauri na kata;
iv)    Kuimarisha ushirikishwaji wa jamii katika Elimu kwa kuanzisha Ushirikiano wa Wazazi na Walimu (UWaWa);
v)    Kutoa Ruzuku ya shughuli za kuongeza pato la shule (IGA –    Income Generating Activities);
vi)    Kuimarisha Uongozi na Usimamizi wa shule kwa kutoa mafunzo kwa Wakuu wa Shule pamoja na matumizi ya vishikwambi katika kutunza na kuwasilisha taarifa na takwimu za elimu katika Mfumo wa Taarifa za Shule (SIS);
vii)    Kutoa Ruzuku ya Maafisa Elimu Kata; na
viii)    Ujenzi wa Vituo Shikizi 121 na ukamilishaji maboma 114     katika shule za msingi unaendelea.

Idara ya Maendeleo ya Miji:-
i)    Kuimarisha utangamano wa Vijiji na Miji (Urban – rural linkage) kwa kuhakikisha kuwa, Mifumo ya Uendelezaji wa Miji na Vijiji (Rural and Urban Systems) inaimarishwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa rasilimali na kuongeza upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi ili kuleta maendeleo sawia;
ii)    Kuratibu, kushauri, kufuatilia na kutathmini matokeo ya utekelezaji wa Sera, Sheria, Miongozo na Kanuni za kisekta kwenye maeneo ya Vijiji na Miji;
iii)     Kuzijengea uwezo Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutekeleza  shughuli za uendelezaji wa Vijiji na Miji;
iv)    Kusimamia na kuziwezesha Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuandaa na kutekeleza Miradi na Programu za uendelezaji wa Vijiji na Miji  na kubainisha fursa za uwekezaji kwenye ngazi ya msingi; na
v)    Kuratibu na kuongoza ukuaji wa Miji Midogo inayochipukia (Emerging Small towns) kutoka Sura ya Vijiji na kuwa Miji.

Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe:-
i)    Kufanya ufuatiliaji wezeshi na tathmini kwa kuboresha utawala bora katika utoaji huduma za afya katika Mikoa na Halmashauri;
ii)    Kutafsiri Sera na Miongozo inayohusiana na maendeleo na mkakati wa fedha wa Sekta ya Afya na ustawi wa jamii;
iii)    Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya huduma za ustawi wa jamii na lishe zinazotolewa katika Mikoa na Halmashauri;
iv)    Kuratibu miradi na programu za sekta ya afya na ustawi wa jamii;
v)    Kuratibu na kufanya ufuatiliaji katika Mikoa na Halmashauri katika kuona kuwa Sera na Kanuni zinazingatiwa;
vi)    Kuratibu na kuhuisha takwimu za kitaifa za huduma za afya na ustawi wa jamii katika Mikoa na Halmashauri;
vii)    Kuratibu na kushauri Mikoa na Halmashauri kuzisaidia jamii kushiriki na kuwa na  umiliki katika utoaji wa huduma za afya;
viii)    Kuratibu, kufuatilia usafi na utunzaji wa mazingira;
ix)    Kuratibu ujengaji uwezo na kutoa msaada wa kiutawala kwa Mikoa na Halmashauri;
x)    Kufanya tafiti kutambua visababishi vya matendo maovu kwa watoto wa mitaani na wanawake;  
xi)    Kupokea na kuunganisha taarifa za miradi na programu kulingana na Mikataba ya Makubaliano iliyopo;
xii)    Kuratibu na kufuatilia huduma za lishe katika Mikoa na Halmashauri; na
xiii)    Kufanya ufuatiliaji wezeshi kwenye Kamati shirikishi za Usimamizi wa Afya za Mikoa kupitia Sekretarieti za Mikoa kuhakikisha zinafanya kazi zake ipasavyo.



Majukumu ya Vitengo

Kitengo cha Uhasibu  na Fedha:-


Kitengo cha Uhasibu na Fedha kinatekeleza majukumu yafuatayo: kusimamia mapato na matumizi ya fedha zote zilizoidhinishwa na Bunge kwa matumizi ya OR-TAMISEMI; kuandaa taarifa za fedha za mapato na matumizi ya (maendeleo na ya kawaida) na kuziwasilisha kwa wakati katika sehemu zinazohusika; kutunza vitabu vya fedha  pamoja na nyaraka mbalimbali,  kuandaa majibu ya hoja za wakaguzi wa Ndani na  Nje, kujenga uwezo Watumishi   wa Kitengo na Ununuzi wa Vitendea kazi.

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani:-
i)    Kufanya ukaguzi wa kawaida wa usimamizi wa mapokezi na malipo, usimamizi wa shughuli za ununuzi na shughuli za utekelezaji wa kazi mbalimbali katika Wizara;
ii)    Kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Wizara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kujua thamani halisi ya miradi iliyotekelezwa na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza;
iii)    Kufanya kaguzi maalum pindi Afisa Masuhuli anavyohitaji huduma ya Kitengo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zilizo chini ya Wizara;
iv)    Kufanya ufuatiliaji wa hoja zinazoibuliwa na wakaguzi katika miradi ya maendeleo; na
v)    Kuratibu vikao vya kisheria vya kamati ya ukaguzi (Audit Committee).

Kitengo cha Mawasiliano  Serikali:-
i)    Kusimamia Uandaaji na Upelekaji wa Habari za OR-TAMISEMI kwa wadau wake;
ii)    Kushirikiana na Idara na Vitengo katika kutangaza miradi mbalimbali inayofanywa na OR-TAMISEMI kwenye vyombo vya habari;
iii)    Kuandaa vipindi vya Redio na Televisheni na kuvitangaza kuhusiana na shughuli zifanywazo na OR-TAMISEMI;
iv)    Kuwa kiungo kizuri cha kuwasiliana na kufanya kazi na vyombo vya habari;
v)    Kuandaa majarida, vipeperushi, mabango na machapisho mbalimbali ya Wizara;
vi)    Kusimamia na Kutoa huduma za Maktaba kwa Watumishi wa Wizara; na
vii)    Kuweka taarifa za Wizara kwenye tovuti ya OR - TAMISEMI.

Kitengo cha Ununuzi na Ugavi:-
i)    Kusimamia shughuli zote za Ununuzi na kufuta mali kwa zabuni;
ii)    Kuratibu kazi za Bodi ya Zabuni;
iii)    Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni;
iv)    Kuratibu vikao vya Bodi ya Zabuni;
v)    Kuandaa mipango ya ununuzi na ufutaji wa mali;
vi)    Kupendekeza ununuzi na ufutaji mali;
vii)    Kuhakiki na kuandaa taarifa za makisio ya mahitaji;
viii)    Kuandaa nyaraka za zabuni;
ix)    Kuandaa matangazo ya fursa za zabuni;
x)    Kuandaa mikataba;
xi)    Kutoa mikataba iliyoidhinishwa;
xii)    Kutunza nyaraka na taarifa za michakato ya ununuzi na ufutaji mali;
xiii)    Kutunza orodha au kumbukumbu ya mikataba yote iliyotolewa;
xiv)    Kuandaa taarifa za ununuzi za kila mwezi;
xv)    Kuandaa taarifa za ununuzi na kuwasilisha kwenye vikao vya Menejimenti;
xvi)    Kuwasiliana moja kwa moja na PPRA katika masuala ya ununuzi;
xvii)    Kuratibu shughuli zote za ununuzi na uondoshaji wa mali; na
xviii)    Kuandaa taarifa zitakapohitajika muda wowote.

Kitengo cha Uboreshaji wa Huduma za Kimenejimenti:-
i)    Kuwezesha uaandaaji na mapitio ya majukumu na miundo ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa Mifumo ya Kimenejimenti na taratibu za utoaji huduma katika Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa;
ii)    Kuibua mbinu bora na kuziasili (Customize) ili zitumike katika    Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali Mitaa;
iii)    Kutathimini ubora wa Miundo, Mifumo na taratibu za kazi kwa ajili ya utoaji huduma bora katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi;
iv)    Kuwezesha na kusaidia katika utekelezaji wa tathmini na mapitio ya kazi kwa ajili ya zoezi la  Kuthathimini ,Kufanya mapitio, na Kupangilia Kazi (JERG -Job Evaluation and Review for Grading) katika RSs, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zake zilipo chini ya OR – TAMISEMI;
v)    Kutoa ushauri wa kitalaam wa kufanya mapitio ya majukumu na miundo ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zake zilipo chini ya OR – TAMISEMI;
vi)    Kuwezesha usimikaji wa Mifumo ya Kimenejimenti katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
vii)    Kusimamia na kufanya tathimini ya utekelezaji wa majukumu na miundo katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa pamoja na Taasisi zilzi chini ya OR-TAMISEMI kutoa ushauri ipasavyo;
viii)    Kuwezesha kufanya maandalizi na mapitio ya Orodha na maelezo ya kazi na kusimamia utekelezaji wake katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Taasisi zilizo chini ya OR-TAMISEMI;
ix)    Kutoa mapendekezo juu ya uanzishwaji na ufutaji wa nafasi za kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja Taasisi zilizo chini ya OR-TAMISEMI;
x)    Kuwezesha ushirikishwaji sekta binafsi na kusimamia utekelezaji wa majukumu katika Sekretariati  za Mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa na kutoa ushauri ipasavyo;
xi)    Kuwezesha na kusimamia utekelezaji wa Mikataba ya Sekta Binafsi katika mipango ya Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zinazosimamiwa na OR-TAMISEMI;
xii)    Kusanifu na kuwezesha usimikaji wa Mifumo ya Ufanisi wa Utendaji kazi na kusimia utekelezaji wake katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zinazosimamiwa na OR-TAMISEMI;
xiii)    Kuwezesha uandaaji na kufanya mapitio ya mikataba ya huduma  kwa mteja kwenye Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi na kusimamia utekelezaji na kutoa ushauri ipasavyo;
xiv)    Kuunda zana za Utafiti wa Utoaji wa Huduma na Tathmini ya  Taasisi, kuzisimika, kufuatilia utekelezaji na kushauri ipasavyo;
xv)    Kuwezesha kutambua maeneo ya huduma kwa ajili ya kuyaboresha / kuyaunda upya;
xvi)    Kuratibu ukusanyaji, uhuishaji na udumishaji wa viwango vya usimamizi wa Benki ya takwimu ikiwa ni pamoja na viwango vya wafanyakazi katika Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi zinazosimamiwa na OR-TAMISEMI;
xvii)    Kuendeleza na kusimika mfumo wa ufuatiliaji na tathmini (M & E), kuweka mikakati na mipango ya kufuatilia utekelezaji wake katika Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Serikali za Mitaa na Taasisi zinazosimamiwa na OR-TAMISEMI;
xviii)    Kuwezesha uandaaji, mapitio, utekelezaji na ufuatiliaji wa mifumo ya utoaji taarifa za utendaji katika Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zinazosimamiwa na OR-TAMISEMI;
xix)    Kufanya udhibiti wa ubora na uhakika wa ripoti za utendaji zilizoandaliwa na kuwasilishwa na Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zinazosimamiwa na OR-TAMISEMI; na
xx)    Kufanya utafiti juu ya hali ya utekelezaji wa mifumo ya ufuatiliaji na tathmini (M & E) na mfumo wa utendaji katika Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Taasisi zinazosimamiwa na OR-TAMISEMI.

Kitengo cha Ukaguzi na Ufuatiliji  wa Matumizi ya Fedha:-
i)    Kuchambua na kuhakiki fedha zilizotolewa katika Mikoa na Halmashauri;
ii)    Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa masuala ya fedha katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
iii)    Kufanya ufuatiliaji wa fedha, tathmini na uhakiki wa matumizi ya fedha hizo.






HISTORY-OF-LOCAL-GOVERNMENT-SYSTEM IN-TANZANIA.pd

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.